MV Merci II Ikianza kuzama katika gati ya kilwa masoko
MV MERCI kabla haijazama
Meli
ndogo ya mizigo ya MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro
imezama katika bandari ya Kilwa masoko. Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina
la Nice Mtega fundi mkuu wa meli hiyo anahofiwa kufa maji baada ya
kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo.Akiongea na Michuzi Blog, Meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary,
alieleza kuwa meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea Songosongo
na kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6
usiku wa kuamkia leo ambapo nahodha wake Charles Kalinga na wasaidizi
wake watatu walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliyekuwa ndani
hajaonekana hadi sasa. Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana. chanzo:issa michuzi
0 comments :
Post a Comment