Licha
ya ripoti za awali kukanusha kupiga marufuku Uislamu, Mamlaka ya Angola
imethibitisha kwamba wamekataa kusajili idadi ya makundi ya kidini ya
Kiislamu na kufungwa misikiti, na kukanusha mateso yoyote dhidi ya
waislamu nchini humo.
"Kuna madhehebu nane ya kiislamu hapa ambayo yote yameomba usajili ambapo hakuna hata moja lililokamilisha hivyo hawawezi kutekeleza imani zao mpaka wakamilishe mchakato", alisema waziri wa mambo ya nje Georges Rebelo Chicoti wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa mabalozi siku ya Ijumaa Kufuatia mlipuko wa dhoruba ya upinzani wa kulishutumu taifa hilo la kusini magharibi ya Afrika kwamba limepiga marufuku Uislamu na kuharibu misikiti.
Mashirika ya dini yanatakiwa kuomba kwa ajili ya kutambuliwa kisheria katika Angola, Chini ya sheria ya Angola kundi la kidini linahitaji kuwa na wanachama zaidi ya 100,000 katika majimbo 12 kati ya 18 ili kupata haki ya kisheria, ya kujenga shule,majengo ya ibada nk.
Takwimu rasmi ya idadi ya Waislamu iliyotolewa na serikali ya Angola ni 90,000, licha ya udhibitisho kutoka kwa Waislamu kwamba idadi yao ni zaidi ya 100,000. Licha ya kufungwa msikiti na kupiga marufuku Mashirika ya Kiislamu, waziri huyo alikanusha mateso yoyote kwa Waislamu. "hakuna mateso yoyote kwa waislamu, hakuna sera ya serikali ya kuwatesa", alisema Chikoti.
Aliongeza kusema kuwa Waislamu wengi hupata leseni ya kujenga maghala ya kibiashara na kisha kutumika maeneo hayo kujenga misikiti bila idhini au sheria kupata leseni kwa ajili ya kujenga maeneo ya ibada.
"Hakuna misikiti iliyojengwa kwa mujibu wa sheria, Katika Angola kuna idadi kubwa ya Waislamu ambao huingia kinyume cha sheria na kisha kufanya ibada zao katika maeneo yao ya biashara", alisema .
Chikoti alisema Angola wanakabiliwa na kufurika kwa wahamiaji haramu na wengi wa hao ni Waislamu.
Makumi ya misikiti nchini Angola imefungwa na kubomolewa na serikali katika mikoa kumi na nane ya nchi hiyo. Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu nchini Angola amesema kuwa, kuna makumi ya misikiti ambayo imefungwa na kubomolewa kwa amri ya serikali ya nchi hiyo.
Televisheni ya Sky News imeripoti kwamba, hatua ya serikali ya Angola ya kufunga na kubomoa makumi ya misikiti ya nchi hiyo imekandamiza na kufanya dhulma dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, serikali ya Angola inabomoa misikiti hiyo kwa kisingizio kwamba,
imejengwa kinyume cha sheria huku ukweli wa mambo ukiwa ni kufanya njama dhidi ya kuenea dini ya Kiislamu katika nchi hiyo.
Aidha misikiti katika mji wa Luanda haijazuiwa hivyo kuleta picha ya uongo kwamba hakuna misikiti iliyofungwa katika nchi hiyo.
Suala la kupigwa marufuku Uislamu nchini Angola limeendelea kutawaliwa na utata kutokana na kuweko habari za kugongana kuhusiana na suala hilo.

Moja ya Misikiti iliyobomolewa |
Waziri wa mambo ya nje wa Angola Georges Rebelo Chikoti |
Blogger Comment
Facebook Comment