Shehe
aliyefariki akizika. Tukio hilo lililowaacha watu na machozi lilijiri
katika Makaburi ya Nonde jijini hapa wakati wa mazishi ya marehemu
aliyejulikana kwa jina la Mayasa Salmini au Bibi Majuto aliyefariki
dunia katikati ya wiki iliyopita.
Aliyekuwa
Shehe Mkuu wa Bakwata Wilaya ya Mbeya, Abubakar Mketo amefariki dunia
mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia kuanguka ghafla makaburini wakati
akitoa mawaidha ya Kiislam ya jinsi waumini wanavyotakiwa kuishi katika
ulimwengu wa dhambi! Inauma sana!
ILIVYOKUWA
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, baada ya kumaliza kuusitiri mwili wa
marehemu Bibi Majuto ndani ya nyumba yake ya milele, Shehe Mketo
alisimama na kuanza kutoa mawaidha kwa waombolezaji waliohudhuria
mazishi hayo akiwaelekeza namna ya kuishi kwa kutii amri za Mungu na
kufuata njia zake kwa vile hakuna anayejua atakufa lini kama ilivyokuwa
kwa marehemu Bibi Majuto.
HEBU MSIKIE
Vyanzo vinadai kuwa, dakika chache kabla ya shehe huyo hajapatwa na mauti alionekana ni mwenye afya njema huku akitoa Neno la Mungu ambalo kila mtu aliyekuwa eneo hilo la makaburi lilimgusa na kujitafakari upya njia zake,
0 comments :
Post a Comment