Maandamano ya mashindano ya michezo ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),jijini Arusha ambayo yanatimua vumbi Uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwanzia tarehe 6 hadi 12 mwezi huu
Wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakifwatilia ufunguzi rasmi wa bonanza la mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kulia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania Idd Azan katikati ni Mh.mbunge Stevin Ngonyani a.k.a Maji marefu
Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akifurahia ushindi baada ya
kushinda nafasi ya kwanza kupeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya
kuibuka mshindi mbio za mita 100 akifuatiwa na Isaac Melley wa Kenya na
Tom Aza wa Uganda aliyeshika nafasi ya tatu.
Wabunge
wa Tanzania Halima Mdee na Ester Matiko waliendeleza ubabe wa bunge la
Tanzania dhidi ya wenzao baada ya kushika nafasi ya kwanza na pili
katika mbio za mita 1,500 na kuwaacha wenzao kutoka Uganda, Kiiza
Winfred na Kangi Elizabeth wakishikilia nafasi za tatu na nne.
Mbunge
Ester Matiko wa Tanzania akijiandaa kukimbia mbio za mita 400,ambapo
aliwatimulia vumbi wabunge wenzake kutoka Kenya, Uganda na bunge la
Afrika Mashariki (Eala).
Kaimu Spika wa bunge la EALA Chris Opoka akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo
Mkuu wa wilaya Arumeru Mhe Nyirembe Munasa afungua
mashindano ya michezo kwa wabunge ambapo aliwataka wachezaji kuacha
kuamini imani za kishirikina na badala yake wamtegemee Mungu kwani
michezo ni kazi kama ajira nyingine
Mkurugenzi
wa KeyMedia Agency Limited Bi Anna Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania
leo jijini Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa
na EALA(East African Legislative Assembly)
Katikati
Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Barbra Lazaro akiwa na wabunge
wa Tanzania leo jijini Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali
yaliyoandaliwa na EALA(East African Legislative Assembly)
Aliyevalia t-shart ya njano ni designer mkuu wa kampuni ya KeyMedia Agency Limited Bahati Masawe akiwa na waheshimiwa Wabunge
Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama akiwa anavuta kamba wakati wa mashindano ya hayo
Mbunge wa Kenya akiwa amebebwa juju baada ya kushinda katika mbio za mita 100
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya akiwa anashangilia kwa furaha katika mashindano hayo
0 comments :
Post a Comment