-->

JINA MUHAMMAD LAONGOZA KUPEWA KWA WATOTO WANAOZALIWA NCHINI UINGEREZA


Utafiti umeonesha kuwa, jina la Muhammad linaongoza kuitwa watoto nchini Uingereza, ambapo jina hilo limeonekana kupewa watoto wengi zaidi wa kiume kati ya waliozaliwa mwaka huu wa 2014 nchini humo.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa katika tovuti ya malezi na mimba ya BabyCentre imeonekana kuwa, jina la Muhammad ni maarufu zaidi kwa watoto wa kiume nchini Uingereza.

Jina hilo ambalo ni la Mtume wa dini ya Uislamu lenye maana ya 'Msifiwa' aliyetukuzwa na Mwenyezi Mungu, lilianza kutumika nchini humo miaka ya 1950 lakini mwaka huu limetumika zaidi.

Jina la Muhammad limeyashinda majina ya Oliver na Jack kwa asilimia 27 na kuwa maarufu zaidi kupewa watoto wa kiume waliozaliwa nchini Uingereza.

Majina mengine ya kiume ya Kiislamu yaliyotumiwa sana nchini Uingereza mwaka huu ni Ali na Ibrahim.

Kwa upande wa watoto wa kike jina la ‘Nur’ limeongoza likifuatiwa na jina la Maryam.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment