Wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014
Wapiganaji
wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo LibyaWapiganaji wa
kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya,
amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Wapiganaji
wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa
Islamic State Septemba 2014 nchini Iraq.Jenerali David Rodriguez
amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi
kwenye kambi zake nchini Libya. Amesema kambi hizo zipo katika hatua za
mwanzo kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona
zinavyoendelezwa.
Libya
imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi
mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali, wanamgambo na makundi ya
kisiasa, wote wakipigania madaraka.
Makundi
mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, hukubaadhi
yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
Wapiganaji
kutoka kikundi cha IS wakipakia mabaki ya kile kinachosemekana kuwa
mabaki ya ndege ya Marekani isiyotumia abiria baada ya kukonga katika
mnara wa mawasiliano huko Raqqa Septemba 23,2014Akizungumza mjini
Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu
uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS."Kikubwa ni
watu wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za
mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya
chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
Watoto
wakikimbia kando ya mlima hukumoshi ukisambaa angani kufuatia mapigano
katika eneo hilo la mji wa Kobani, wakati majeshi yanayoongozwa na
Marekani kushambulia wapiganaji wa Islamic StateWaandishi wa habari
wanasema katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi,
wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi
vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea
nyumbani(Libya).
Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.
Benghazi,
mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa
Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao
vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo
Marekani
imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga
dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.
SOURCE:MATUKIO NA VIJANA
SOURCE:MATUKIO NA VIJANA
0 comments :
Post a Comment