-->

MUNIRA MADRASA YAFANYA SHEREHE ZA KUUPOKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM 1435 HIJRIYA




Hatimaye Taasisi ya Munira Madrasa imefanya sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu 1435 HJR

Sherehe zimemalizika hivi punde katika viwanja vya Madrasa hiyo vilivyopo Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.

Katika sherehe hizo zilizo hudhuriwa na wazazi,walezi na wanafunzi,michezo mbalimbali ilichezwa kwa kuwashirikisha watoto wa jinsia na rika zote.

Kivutio kikubwa kilikuwa ni mchezo wa kuunda namba ya 1435 HIJRIYYAH na mchezo wa kugombea kukalia kiti huku washindi wakikabidhiwa zawadi za matunda.

Aidha kupitia sherehe hizo wanafunzi wa Munira Madrasa walikabidhiwa ripoti zao baada ya kumaliza mitihani ya mwaka waliyoifanya hivi karibuni.

Katika tukio hilo mwanafunzi Maryam Muhammed alikuwa ni mshindi wa jumla ambapo yeye na washindi wenzake walizawadiwa pesa taslim.

Akiongea katika sherehe hizo,mgeni Rasmi Sheikh Ramadhan Kwangaya aliwataka wazazi kuunga mkono juhudi za walimu huku akiwataka waalimu hao kuongeza bidii katika utendaji wao na kutokata tamaa kwa changamoto zinazo wakabili. 

 
 MARYAM MUHAMMAD AMBAYE NI MSHINDI WA JUMLA AKIWA NA MAMA YAKE MUDA MFUPI BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI

 


 













 


Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment