Upinzani nchini Ukraine unamatumaini kuwa waandamanaji hadi alfukumi watajitokeza leo(01.12.2013)Jumapili na kutoa msukumo mpya kudai rais Viktor Yanukovich ajiuzulu kutokana na mzozo wa uhusiano na Umoja wa Ulaya.
Maandamano mjini Kiev
Vyama vikuu vitatu vya upinzani vimesema vinaanzisha , "kikosi cha taifa
cha upinzani" baada ya polisi wa kuziwia ghasia kuwatawanya waandamanji
kwa kutumia nguvu na kuwajeruhi watu kadha jana Jumamosi.
Mkutano huo wa waungaji mkono upinzani ulivunjwa na polisi waliotumia
virungu ambao waliwashambulia kiasi ya waandamanaji 1,000 katika uwanja
wa uhuru katika mji mkuu Kiev mapema jana Jumamosi asubuhi(30.11.2013).
Maandamano mjini Kiev
Kiasi ya watu 10,000 walikusanyika katikati ya mji wa Kiev usiku wa
Ijumaa na kusema Yanukovich ajiuzulu baada ya rais huyo kukataa kutia
saini makubaliano ya kisiasa na kibiashara pamoja na Umoja wa Ulaya.
Maandamano zaidi
Upinzani umetoa wito wa kufanyika maandamano mapya leo katikati ya mji
wa Kiev baada ya polisi kuzingira uwanja huo wa uhuru kwa kuweka uzio wa
chuma.
"Tunaweza na tunapaswa kuwaondoa viongozi hawa," bingwa wa dunia wa
ngumi Vitali Klitschko , kiongozi wa chama cha UDAR amewaambia waungaji
mkono upinzani wapatao 10,000 siku ya jumamosi, na kutangaza maandamano
mapya.
Vitali Klitschko kiongozi wa chama cha UDAR
"Tunapaswa kujitokeza na kuonesha kuwa hatutawaruhusu kutudhalilisha,
tutasimama na kudai haki zetu," ameuambia mkusanyiko huo karibu wiki
moja baada ya maandamano makubwa ya umma kuzuka nchini Ukraine kufuatia
uamuzi wa maafisa kuachana na mpango wa kutia saini makubaliano na Umoja
wa ulaya ambayo yangeiweka jamhuri hiyo ya zamani ya Umoja wa Kisovieti
katika njia kuelekea kujiunga na Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya
umeishutumu Urusi kwa kuipa mbinyo Ukraine, nchi ambayo inategemea kwa
kiasi kikubwa gesi kutoka Urusi, na kujitoa kutoka katika makubaliano
hayo.
Matumizi ya nguvu na vitisho
Jana Jumamosi , Lithuania ambayo inashikilia uongozi wa Umoja wa Ulaya
kwa sasa imesema matumizi ya nguvu "hayavumiliki" na mkuu wa sera za
mambo ya kigeni wa Umoja huo Catherine Ashton pamoja na kamishna wa
upanuzi wa Umoja huo Stefan Fuele wametoa wito wa kufanyika uchunguzi.
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa EU, Catherine Ashton
"Matumizi ya nguvu na vitisho havina nafasi katika Ukraine ya leo,"
ameongeza msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Marekani, Jen Psaki
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty
International limetoa wito kwa maafisa nchini Ukraine kutimiza wajibu
wao wa kulinda haki za binadamu.
Jana Jumamosi, Yanukovich alisema katika taarifa kuwa, "amefadhaishwa
mno" na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji na ameapa kuwa
waliohusika wataadhibiwa.
CHANZO:MY VOICE
Blogger Comment
Facebook Comment