-->

HIVI NDIVYO KOCHA MPYA WA SIMBA ALIVYOPOKELEWA


Mashabiki wa Timu ya Simba, wakimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini jana machana.




Mara kadhaa kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongoni na hata wachezaji wa Klabu zetu kubawa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha mpya ama kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea kukosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu husika, anaweza kutimulia ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.


Wakati umefika sasa kwa Klabu zetu kufunguka kifikra na kuwa na upeo wa kufikiri ili kuziendeleza klabu zetu, kwa kuwaachia makocha waweze kufanya yale yanayostahili bila kuingiliwa na viongozi ama watu flani kwa pesa zao ama umaarufu wao katika klabu. 


Huko nyuma walikwishapokelewa makocha kadhaa kama alivyofanyiwa kocha huyu leo na waliondoka kimya kimya huku wengine wakiondoka klabuni kwa mafalakano na viongozi wa klabu.

Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar leo.

Akipata menu.....

Kocha huyo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Simba wakati alipotembelea na kukagua uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo wa Kinesi.Picha kwa Hisani ya Lenzi ya Michezo
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment