Viongozi wa Waislamu na Wakristo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wameungana ili kuzuia kuuliwa raia nchini humo.
Askofu Mkuu Dieudonne Nzapalainga, na Imam Omar Kobine Layama, kiongozi wa Waislamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameamua kushikamana ili kuzuia kutokea mapigano zaidi kati ya wafuasi wa dini hizo kufuatia kushadidi mapigano ya kikabila na kidini nchini humo yaliyosababisha kuuliwa watu wengi.
Waasi wa zamani wa Seleka Jumapili wiki hii walipigana na wanamgambo wa Kikristo na kushambulia makazi ya kiongozi wa waasi hao wa zamani katika eneo la Galabadja na kufanikiwa kulidhibiti eneo hilo.
Hatua hiyo imeibua hofu kwa wakazi wa eneo hilo na kuwafanya wakimbilie majumba ya ibada kwa ajili ya kupata hifadhi wakihofia kushadidi mapigano kati ya pande mbili hizo.

0 comments :
Post a Comment