Kwa akali Waislamu 23 wameuawa juzi mjini Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kushambuliwa wakiwa ndani ya msikiti. Mauaji hayo yamefanywa na kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti Balaka.
Sheikh Muhammad Wasil Imam wa Masjidul Noor mjini Bangui amesema kuwa, Waislamu hao wameuawa baada ya kukimbilia Msikiti humo kwa lengo la kujipatia hifadhi. Sheikh Muhammad Wasil ameongeza kuwa, wanamgambo hao wa Anti Balaka waliwauwa Waislamu hao kwa kuwakatakata na wengine kuwachinja kama kuku kwa kutumia mundu. Imam wa Masjidul Noor ameongeza kuwa, wanamgambo hao wa Kikristo hawakuwa na huruma hata kwa wanawake na watoto, kwani wote waliokuwa wamejificha Msikitini humo waliuawa kinyama na miili yao bado iko pambizoni mwa Msikiti huo. Ameongeza kuwa, wahanga hao watazikwa pambizoni mwa Msikiti, baada ya majeshi ya nchi hiyo kukataa kutoa ruhusa ya kuzikwa kwenye makaburi ya Waislamu yaliyoko nje ya Bangui.
chanzo:sauti ya tehran

0 comments :
Post a Comment