Mwanamke
wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na kilo 1.1 za madawa ya
kulevya aina ya heroin alizokuwa amezihifadhi tumboni mwake,baada ya
kukamatwa huko Macao, nchini China. Dawa hizo zenye jumla ya vidonge 66
vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani 137,720.
Mwanamke
huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne
iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni
mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
Pichani
ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na
kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Macau, Disemba 19, 2013.
CHANZO:ISSAMICHUZI
0 comments :
Post a Comment