Google imeifungia akaunti ya Mwanasiasa
wa kiholanzi mwenye chuki zaidi na uislamu Geert Wilders, baada ya
kutolewa malalamiko dhidi yake kutumia akaunti hiyo kueneza chuki ya
kupambana dhidi ya Uislamu.
Malalamiko hayo yaliwasilishwa na Mohammed Rabbae kwa niaba ya Baraza la taifa la Morocco kwa kutumia vibaya huduma za Google.
Malalamiko ya Rabbae yalitokana na malalamiko ya watu wengi dhidi ya Wilders kufuatia kutoa stika wiki iliyopita iliyosomeka kwamba, 'Uislamu ni uongo, Muhammad ana kosa la jinai, Qurani ni Sumu'.
Katika
kujitetea mwanasiasa huyo alisema hakumaanisha ubaya dhidi ya uislamu.
Hata hivyo amefungua akaunti nyingine mpya. Mwaka 2008 alitoa makala ya
dakika 15 inayoshutumu Qurani kwa uchochezi wa vurugu.
Wilder ndiye mtu anayetajwa kwa sasa kuongoza kuwa na chuki zaidi dhidi ya Mtume Muhammad ï·º na dini ya Uislamu.
Mshirika wake wa karibu sana aliyekuwa akipinga zaidi ni Arnoud van doorn ambaye mwanzoni mwa mwaka huu amesilimu.
Kabla ya kusilimu Van doorn ndiye aliyetajwa kuwa ndiye aliyeongoza kwa kumchukia Mtume Muhammad ï·º na Uislamu.
Kabla ya kusilimu Van doorn ndiye aliyetajwa kuwa ndiye aliyeongoza kwa kumchukia Mtume Muhammad ï·º na Uislamu.
Chanzo:Ahbaabur
Geert Wilders |
0 comments :
Post a Comment