-->

CHAMA CHA MAPINDUZI TANZANIA CHAWASHA MOTO SHINYANGA


SHINYANGA YA ZIZIMA,MWIGULU NCHEMBA NA MH;MASELE WAWASHA MOTO,HENRY MATATA AMLIPUA SLAA KWA KUMWAGIA TINDIKALI MUSA TESHA.

CHADEMA WAFICHA MIFUKO YA CEMENT 200 NYUMBANI KWA MADIWANI ILI KUKWAMISHA MAENDELEO.
Endelea hapa
Mh.Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba akipongezwa na Mh.Masele Mbunge wa Shinyanga Mjini hii leo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuitumikia CCM kwa moyo wote na anavyoipigania serikali yake Bungeni hasa kuwa mstari wa mbele kuzungumza ukweli kuhusu mafanikio ya Serikali ya CCM na namna wapinzani wanavyohadaa watu kwa kuzungumza mambo yasiyotekelezeka kwa Watanzania hususani Uhalalishaji wa Gongo kwa watanzania ili serikali iongeze mapato.

Mh.mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Kambarage hii leo Tar.29/12/2013 katika moja ya ziara za Mbunge wa jimbo hilo Mh.Masele ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na miradi ya maendeleo.Mh.Mwigulu Nchemba akiwa Shinyanga pia alifanikiwa kufanya vikao vya ndani na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi WIlaya ya Shinyanga mjini na Mkoa,Pia alitumia muda wake kukutana na Mabalozi wa wilaya ya Shinyanga mjini.Pamoja na mambo mengine,Mh.Mwigulu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu aliwaomba viongozi wa CCM wilaya kusimamia miradi ya maendeleo vizuri(Ujenzi wa Zahanati,Shule,matundu ya Vyoo ya wanafunzi,.Soko,Jengo la NSSF) ambayo yote hayo ni jitihada za Mh.Masele kwa wananchi wake wa Shinyanga Mjini.
Naibu Katibu Mkuu kupitia vikao vyake vya ndani na kwenye Mkutano wa hadhara amewasisitiza Wananchi wa Shinyanga Mjini kumpatia ushirikiano Mh.Masele katika shughuli zake zote za maendeleo,Ikumbukwe Mh,Masele ni Naibu wa Wizara ya Nishati na Madini,Hivyo basi anakazi nyingi za serikali na za jimboni kwake,Wananchi na viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa kuhakikisha wanampatia Mbunge huyo Ushirikiano wa kutosha ilikuhakikisha Ilani ya chama cha Mapinduzi inafanikiwa vizuri.

Mh.matata Meya wa Ilemela pia alipata nafasi ya kusalimiana na Wananchi wa kata ya Kambarage Shinyanga Mjini.Kubwa alilosema Mh.Matata ni kwamba Kitendo cha Kumwagiwa Tindikali kwa Kijana MUsa Tesha pale Igunga ni mpango wa Dr,slaa na ndiye aliyefadhili hilo Swala,Vijana waliofanya mchezo huo walifika kwake Mwanza kwa maagizo ya Slaa kwamba awape kazi kwenye Meli zake Matata zinazofanya kazi Tanzania na Uganda bila kujua kuwa Vijana wale ndio waliomwagia Tindikali kwa Tesha Igunga,Baada ya Kukosana na Slaa,ndipo Vijana wale wakakimbia kwa Matata kwa kutoroshwa na Dr.slaa.Hivyo CHADEMA hawafai,Kwa sasa kuna Vita kati ya Wakaskazini na Watanzania wote.

Pia Mh.Matata amesema ZItto Kabwe atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA hatakama Wachaga hawataki,ZItto Kabwe ni kijana jasiri,Msomi na mwelewa.Wakati CCM wanavua na kuondoa Mawaziri Mizigo,CHADEMA wanaondoa Viongozi Bora na Kubakisha Mizigo Kama Lema,Wenje,Mbowe,Sugu n.k alisema Matata

Katika hali isiyoyakawaida Madiwani wawili wa kata zinazongozwa na CHADEMA Shinyanga Mjini wamekalia mifuko 200 ya Cement aliyotoa Mh.Masele kwaajili ya Ujenzi wa Soko na Zahanati.Tukio hilo limetokea wakati Mh.Masele miezi 3 iliyopita aligawa mifuko ya CEMENT kwa kata zake zote kulingana na Mahitaji yao,Katika kata ambazo CHADEMA wanaongoza waliomba mifuko ya CEMENT 100 kila kata kwaajili ya Ujenzi wa SOko na Zahanati,Vivyo hivyo kwa Kata za CCM ikiwamo ya kambarage walipewa mifuko 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati na matundu ya Choo ya shule.

Huku Kata zingine zinazongozwa na CCM zikiwa zimekamilisha ujenzi huo kwa asilimia zaidi ya 80,kata zinazongozwa na CHADEMA mifuko imepatikana Nyumbani kwa madiwani hao bila kutoa sababu za Msingi ni kwanini wameshindwa kujenga maeneo husika kutokana na maombi yao.Katika ziara yake Mh.Masele ameagiza Madiwani wa kata husika wawajibishwe na wananchi wao kwa kukwamisha miradi ya maendeleo kwa maksudi(hujuma).Vile vile amejitolea kusaidia kila kata kumalizia ujenzi wa Zahanati,Soko na matundu ya Shule,Kwa awamu ya kwanza amekuja na Nondo kwaajili ya Madirisha na milango na ameshaanza kugawa kwa kata zile zilizokamilisha zoezi la ujenzi wa miradi yao isipokuwa zile za CHADEMA.Wilaya ya Shinyanga mjini inajumla ya kata 17 na kata 6 zinaongozwa na Upinzani.
Ingia hapa kuendelea>>http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/577324-picha-mwigulu-masele-waunguruma-shinyanga-matata-amlipua-slaa-kwa-tindikali-cdm-waficha-cement.html#post8232409
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment