-->

UGANDA WAPIGA MARUFUKU VAZI LA KIMINI NCHINI HUMO

Bunge la Uganda limepitisha muswada unaopiga marufuku wanawake kuvaa sketi fupi, pamoja na vitendo vinavyochochea ngono, limeripoti gazeti binafsi la Daily Monitor.

Muswada huo uliopendekezwa mwaka 2011 unapiga marufuku pia video za ngono, miziki na hata ngoma zinazochochea vitendo hivyo. 

Serikali ya Uganda inasema kuwa, picha za ngono zimekuwa tatizo kubwa kwa jamii na huchochea jinai za ngono dhidi ya wanawake na watoto kama vile kubakwa na kutumiwa watoto wadogo katika ngono. 

Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya ni marufuku kuacha wazi baadhi ya sehemu za mwili kama vile makalio, mapaja na matiti na kutenda kitendo chochote kinachochoea hisia za ngono.

Hata hivyo wako walioikosoa sheria hiyo wakisema kwamba, ponografia ina maana pana na sheria hiyo inakinzana na tabia ya Waganda ya kuvumilia mazoea na desturi tofauti.

Takwimu za ukimwi nchini Uganda ni asilimia 7.2 sawa na watu milioni 1.4 ya waganda wote wenye ugonjwa wa ukimwi. Mwaka 2011 watu wapatao 62,000 nchini Uganda walifariki kwa ukimwi.

Sheria na taratibu za kiislamu ni haramu mwanamke kuacha wazi sehemu za mwili wake isipokuwa uso na viganja vya mikono. 

Utafiti unaonesha sehemu ambazo wanawake wamekuwa wakivaa mavazi ya stara, vitendo vya ngono na maambukizi ya ukimwi yamekuwa kwa kiwango kidogo kulinganisha na maeneo ambayo wanawake wanavaa mavazi yasiyo ya stara.

Bunge la Uganda
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment