WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala na anapumua kwa msaada wa mashine.
Mwanaspoti jana Jumatatu mchana lilimshuhudia
Lunyamila akiwa amelala katika kitanda namba 18 cha wodi ya wanaume
katika hospitali hiyo ya mkoa wa kitabibu wa Kinondoni.Edibily Lunyamila akichanja mbuga.
Kwa mujibu wa Daktari, Madirisha Pascal,
aliyempokea na kumpatia huduma ya kwanza winga huyo wa zamani, Lunyamila
anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua
vizuri.
“Sasa anapumua kwa msaada wa mashine na bado
tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,”
alisema Pascal.
Ndugu wa Lunyamila aliyemfikisha hospitali hapo
aitwaye Lameck John, aliliambia Mwanaspoti kwamba Lunyamila alianza
kujisikia vibaya juzi Jumapili na jana Jumatatu asubuhi hali yake
ilibadilika ndipo alipomwahisha hospitali.
Winga hatari wa zamani klabu ya Dar es
salaam Young Africans Edibily Jonas Lunyamila, akimtoka beki wa zamani
wa Simba Mathias Mulumba, katika mchezo wa fainali ya kombe la Hedex
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika miaka ya tisini, na
hii ilikuwa ni muda mfupi baada ya Lunyamila kutua nchini toka nchini
Ujerumani alikokuwa amekwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa, na siku hii akiwapiga Simba moja kati ya mabao mawili na
lingine likifungwa na Bakari Malima kufuatia kona ya Lunyamila.
“Alikuwa analalamika hawezi kupumua na kifua
kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo
tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck.
Lunyamila hakuweza kuzungumza na mwandishi wa habari hii kwani alikuwa amelala.
Lunyamila aliyeichezea Yanga kwa mafanikio katika
miaka ya 1990, amewahi kuisaidia Yanga kucheza hatua ya makundi ya Ligi
ya Mabingwa Afrika mwaka 1998.http://www.mwanaspoti.co.tz
0 comments :
Post a Comment