Siku moja baada ya
kupokea kipigo cha kihistoria cha 5-0 kutoka kwa Liverpool wakiwa kwenye
uwanja wao wa nyumbani, klabu ya Tottenham Hotspur imemtimua kocha mkuu
wa timu hiyo Andre Villas Boas.
Tottenham ambao walikuwa
ndio timu iliyotumia fedha nyingi kufanya usajili wakati wa dirisha la
usajili, wakitumia zaidi ya paundi millioni 100, wameanza vibaya msimu
huu na hivyo kufikia maamuzi ya kumtimua AVB ambaye alijiunga na timu
hiyo miezi takribani 18 iliyopita.
Majina ya Luis Enrique
na Fabio Capello yameanza kutajwa kuja White Hart Lane kuchukua nafasi
inayoachwa wazi na kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Porto.
0 comments :
Post a Comment