-->

WANAFUNZI WA CHUO KIKONGWE DUNIANI CHA AL AZHAR WAANDAMANA

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/6c2a1b5749cd299679a86a9cc079c34f_XL.jpgMapigano mapya yamejiri kati ya vikosi vya usalama vya Misri na wanachuo waliokuwa wakiandamana katika Chuo Kikuu cha al Azhar huko Cairo, mji mkuu wa nchi hiyo.
Mapigano hayo yametokea leo Jumapili baada ya wanachuo kuandamana kupinga serikali ya mpito ya Misri iliyoingizwa madarakani na jeshi. Jumamosi wiki hii wanachuo wawili wa al Azhar waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati vikosi vya usalama vilipozuia maandamano ya wanafunzi wa chuo hicho.
Kitivo cha masomo ya biashara cha Chuo Kikuu cha al Azhar huko Cairo kilichomwa moto hapo jana, hata hivyo wanachuo walikadhibisha kuwa wao ndio waliokichoma. Maandamano mengine yalishuhudiwa hapo jana katika miji ya al Khusus, Beni Suef na Alexandria dhidi ya watawala wa kijeshi wa Misri.
Wakati huohuo gazeti la al Masriyun limetoa matokeo ya uchunguzi wa maoni na kuandika kuwa Muhammad Morsi Rais wa Misri aliyepinduliwa na jeshi ni shakhsia wa mwaka 2013.
Morsi ametangazwa kuwa shakhsia wa mwaka huu wa 2013 huko Misri kufutia uchunguzi wa maoni uliofanyika kwa muda wa siku kumi huko Misri  na kuwashinda mahasimu wake Hamdin Sabahi, mgombea wa zamani wa kiti cha urais na Abdulfatah al Sisi, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.
CHANZO:RADIO IRANI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment