-->

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA SIKU 45 JELA KWA KOSA LA KUSALI KWENYE MSIKITI ULIOBOMOLEWA

PICHA KUTOKA MAKTABA/SALA YA EID IL FITR MKOANI MOROGORO
MAHAKAMA ya Bahrain imemhukumu kijana mmoja wa nchi hiyo kifungo cha siku 45 jela kwa kosa la kusimamisha Sala katika msikiti uliobomolewa na utawala wa kifalme wa Aal Khalifa nchini humo.



Taarifa kutoka Manama zinaeleza kuwa, Ali Hashim Ali alipatikana na hatia hiyo ya kusali katika Msikiti wa Muhammad Amir al Barighi ulioko nje kidogo ya Manama mji mkuu wa nchi hiyo. 


Kikosi cha Usalama nchini Bahrain kwa muda wa wiki mbili kimekuwa kikilizingira eneo la msikiti huo uliobomolewa na kuwapiga marufuku Waislamu kutekeleza ibada zao katika eneo hilo. 


Hatua ya utawala wa kifalme wa Aal Khalifa kuwakataza Waislamu wasitekeleze ibada ya sala katika eneo hilo imewakasirisha wananchi wa nchi hiyo ambayo zaidi ya asilimia 99. 8 ya wakazi wake ni Waislamu.


Inafaa kukumbusha hapa kuwa, tokea ilipoanza harakati ya wananchi wa Bahrain mwezi Februari 2011 hadi sasa, mamia ya wapinzani wa serikali wameuawa na kutiwa mbaroni na zaidi ya misikiti 50 imebomolewa na askari usalama ya nchi hiyo. 


Vilevile utawala huo wa kifalme umetakaa katakata kukarabati au kujenga upya misikiti hiyo iliyobomolewa.http://kiswahili.irib.ir
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment