
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Felchesmi Mramba amezungumza kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema ‘ni kweli kama tulivyotangaza mgao wa Umeme kuchukua siku kumi kutokana na matengenezo yale ya songosongo na kazi imeshakamilika na mgao umekwisha, nataka kuwapa habari hizi njema za furaha watumiaji wa Umeme kwamba adha waliyoipata imefikia mwisho’
millardayo.com : Vipi kama kuna watu bado wataendelea kulalamika kupata mgao wa Umeme?
Mramba : Kama mtu akiona kuna mgao naomba nitoe namba yangu, yeyote atakaeona mgao anipigie 0767 042 009… bado tunatumia mitambo ileile ya Songosongo pamoja na mitambo ya mafuta ya kwetu huku ndio tunatumia, kidogo hali ya maji sio nzuri lakini maji kidogo yaliyopo yanachangia kwa hiyo tukiunganisha nguvu zote hizo na mitambo ya dharura ya mafuta ndio tunapata umeme wa kuwapa Watanzania’
CHANZO:MILLARD AYO
Blogger Comment
Facebook Comment