Baadhi
ya wakazi wa Mivinjeni ufundi Kurasini wamefunga barabara ya kilwa
jijini dar es salaam kwa muda wa saa mbili wakishinikiza kulipwa hundi
zao na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna
Tibaijuka na kusababisha foleni kubwa ya magari.
Wakazi hao wamesema kuwa serikali ilikubaliana na mwekezaji kuwalipa pesa zao na kutaftiwa viwanja huko kibada lakini cha kusikitisha zoezi la ulipaji hundi lilisitishwa hapo jana mpaka waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Prof Anna Tibaijuka atakapotoa tamko lini walipwe.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiongea kwa njia ya simu na Itv amemuagiza Mkuu wa Wilaya watu hao kutawanywa na yeyote atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria kwani si taratibu sahihi kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara hiyo ambao hawahusiki.

0 comments :
Post a Comment