Mkunga huyo akionyesha mkeka unaotumika kuwatandikia wajawazito wanaokuja kujifungulia katika kliniki yake
MKUNGA akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa
aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama
wajawazito.
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA
ERICK mwenye umri wa miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya
chunya ,amejifungua mtoto jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.
Mkunga aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa
MBUYUNI wilaya ya chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa
alasiri agosti 13 mwaka huu,mara mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga
huyo na mumewe aitwaye BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye umri wa miaka thelathini
na tano
MATRIDA amesema huo ni uzao wake wanne na
kwamba alishangazwa na kiumbe hicho ingawa wakati anajifungua hakupata
tatizo lolote na pia alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na
alisikitishwa kupata hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye
vidole vinne na miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.
Kwa upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa
katika kondo lake na chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa
mwanamke huyo na pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la
kwanza mwanamke alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili
mwaka huu mwezi wa tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu
kwa hiyo hili ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.
Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia
yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa
kijiji cha MBUYUNI bwana CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji
MICHAEL SANZIMWA ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo
kuondoa kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.
Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae
ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani
za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
Na Ezekiel Kamanga Mbeya yetu
|
0 comments :
Post a Comment