PICHA BAADA YA MABOUMU YA MACHOZI KUPIGWA
Leo kwenye kongamano la kuita umoja wa waislam katika yanayo wakabili waislam mkoani Morogoro..Kongamano lillienda vizuri likiwa limepambwa na mashekh wakubwa wakubwa kama vile Riko,Mwaipopo,Kondo pamoja na shekh Ponda.Shekh ponda alikuwa wa mwisho kutoa mawaidha na aliaga waislam ili aweze kuelekea Msikiti wa Mungu mmoja hivyo waislam walitaka kumsindikiza Shekh Ponda mpaka Mskiti wa mungu mmoja.Maaskari waliovalia nguo za fild force wakiwa kwenye defender waliingia na kuanza kuifuata gari kwa nyuma.Waislam waliendelea kuizunguka gari ya Shekh ponda ila maaskari walianza kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi kisha kuifukuza gari ya shekh Ponda.Sikubahatika kushuhudia nini kiliendelea kutokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa na maaskari hao lakini dakika chache baadae nilipata taarifa ya kwamba amepigwa risasi ya bega na amepelekwa hospitalini.....endelea kutembelea blog ili ujue nini kinaendelea kwa Shekh Issa Ponda amabae inasemekana yupo Hospitali tayari kupata tiba.
Hizo ni picha za mawingu moshi au mawingu mdaa!
ReplyDelete