-->

SOMA RIPOTI YA MADAKTARI KUHUSU HALI YA SHEKH PONDA HAPA

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAJERAHA YA SHEIK PONDA ISSA PONDA 

Dar es salaam  12/8/2013 

Sheikh Ponda issa ponda (54) alipokelewa hapa taasisi ya ya tiba ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30 adhuhuri akitokea hospitali ya taifa muhimbili 
baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya 
bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma 
madaktari wetu walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe kipimo cha x-ray ili ubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha 
tathimini ya madaktari baada ya kupata majibu ya x/ray ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana 
vivyo hivyo kidonda hakikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo  
KWA HIYO 
1-kufwatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla kabla ya kufikishwa moi imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa na kitu gani 
2-kipimo cha x-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana  
3-hivyo basi sheikh ponda issa ponda anaendelea n matibabu baada ya upasuaji . 
                                            mkurugenzi mtendaji 
                   taasisi ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment