-->

HAYA NDIYO YALIYOJIRI KWENYE KONGAMANO LA MWEMBE YANGA KUHUSU KUPIGWA RISASI KWA SHEKH PONDA

Leo Waislamu walikusanyika kwa
wingi katika viwanja vya Mwembe
Yanga, Temeke Jijini Dar es Salaam
kuwasikiliza masheikh wanatoa
tamko gani kuhusu kadhia ya
kujeruhiwa Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda.
Uwanja ulikuwa umefurika waumini
waliokuwa na hamu kubwa ya
kusikiliza kile kitakachosemwa na
viongozi wao.
Tulibahatika kuhudhuria kuanzia
mwanzo wa shughuli mpaka mwisho,
ingawa hatukuweza kuwaletea
yaliyokuwa yakiendelea moja kwa
moja kutoka uwanjani kutokana na
sababu zilizokuwa nje ya uwezo
wetu.
Hata hivyo, muda si mrefu shughuli
imekamilika. Mwitikio ulikuwa
mkubwa na watu walikuwa wengi
sana, uwanja wa Mwembe Yanga
ulifurika hasa.
Sheikh kutoka Morogoro, aliwaelezea
tukio zima la kupigwa risasi kwa
Sheikh Ponda, jinsi alivyowatoroka
Polisi na kile kilichofanywa na jeshi
hilo katika uficha ukweli.
Baada ya Sheikh kutoka Morogoro,
ilifuatia salamu ya Sheikh kutoka
Zanzibar ambaye alielezea kadhia
nzima ya safari ya Sheikh Ponda
visiwani Zanzibar na yale
aliyoyatamka dhidi ya dhulma
iliyofanywa na serikali ya visiwa
hivyo kwa masheikh mbalimbali.
Mpaka sasa kadhaa wapo ndani na
huu ni mwezi wa 10 hawajapewa
dhamana. Aliwaeleza Waislamu
kuwa tayari wana muungano wao,
ambao ni Muuungano wa Uislamu, na
hivyo hawahitaji muungano
ulioasisiwa na Mzee Nyerere na
Mzee Karume.
Aidha, alisema kuwa muungano wa
Uislamu ni imara zaidi kuliko
muungano huu unaolazimishwa na
watawala.
Pamoja na mambo mengine
alizungumzia tukio la kumwagiwa
tindikali kwa wasichana wawili, raia
wa Uingereza. Alieleza kuwa, kwa
mujibu wa gazeti la Telegraph la
Uingereza, matukio hayo
yameongezeka huko nchini
Uingereza, na hivyo kuna uwezekano
kuwa wahusika wa tukio hilo
wanatoka huko huko Uingereza.
Baadaya swala ya Alasiri, ilitolewa
mada kuhusu harakati za Sheikh
Ponda, msingi na malengo yake,
pamoja na kile kilichompata Sheikh
huyo.
Waislamu walikuwa na msisimko na
hamasa ya ajabu mno ambayo muda
mwingi watoa mada walilazimika
kukatisha mada zao ili kupisha sauti
za Takbirah zilizokuwa zikihanikiza
uwanjani hapo.
Baada ya mada hiyo, uliwadia wakati
wa tamko lililotolewa na Amiri wa
Wahadhiri Tanzania, Sheikh Kondo
BUngo. Yafuatayo yalikuwa katika
tamko hilo la Mwembe Yanga:
1- Waislamu wanatambua kuwa
Sheikh Ponda alipigwa risasi na
Polisi kwa lengo la kumuua.
2- Waislamu wanataka Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Morogoro
awajibishwe, ikiwa ni pamoja na
kupelekwa mahakamani. Hasa
ikizingatiwa kuwa wakati akiongea
na vyombo vya habari vya ndani,
alikanusha tuhuma za polisi
kutekeleza kitendo hicho, lakini
alipoongea na vyombo vya habari
vya nje alikiri kuwa polisi walimpiga
risasi Sheikh Ponda, kama
ilivyonukuliwa na vyombo hivyo.
3- Kamanda wa operesheni ya
kumkamata na kumjeruhi Sheikh
Ponda, pamoja na askari aliyepiga
risasi wanatakiwa kuwajibishwa na
kushitakiwa.
4- Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.
Emmanuel Nchimbi ajiuzulu.
5- Waislamu hawaitaki tume ya
polisi, bali wanataka tume huru
itakayochunguza tukio hilo, kwa
sababu Polisi ni waongo, na
Waislamu hawana imani nao tena.
Aidha, Polisi ni watuhumiwa, hivyo
hawawezi kujichunguza kisha
wakatenda haki.
6- Waislamu wanatangaza kuwa adui
yao mkubwa kwa sasa ni serikali ya
CCM, na hivyo wanakusudia kuitia
adabu. Kampeni za kuitia adabu
zinaanza sasa hivi mpaka mwaka
2015 wakati wa uchaguzi mkuu.
Iwapo hayo hayatatekelezwa,
Waislamu wametangaza kuchukua
hatua stahiki itakayoifanya iwe
mwisho wa kudhulumiwa katika nchi
hii.
Ndugu wadau, kwa mukhtasari hayo
ndiyo yaliyojiri katika Viwanja vya
Mwembe Yanga, ambapo sisi
wenyewe tulikuwa mashuhuda.
Ahsanteni sana... na tunaomba radhi
kwa usumbufu.
SOURCE:ISLAMIC FORUM PAGE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment