

Akizungumza na Habarimpya.com kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Camillius Wambura amesema kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtengo na walinzi wa Kampuni ya Security Group.

"Mtuhumiwa huyo raia wa Bulgaria anaitwa Todor Peev Peev alikamatwa na kadi za ATM 21 na tayari akiwa ameshatoa tsh 200,000 kwenye tawi hilo,tunaendelea kumhoji ili tujue ni jinsi gani aliweza kupata kadi hizo, taarifa za benki hiyo kupitia kamera zilizofungwa ndani ya ATM pia imetuonyesha kwamba mtuhumiwa huyo amekuwa akionekana kila mara katika tawi hilo akitoa pesa"alisema Wambura.
SOURCE:HABARI MPYA
0 comments :
Post a Comment