Mkurugenzi TCRA Profesa John
Nkoma
Mkurugenzi TCRA Profesa John
Nkoma amesema mamlaka hayo yameitambua rasmi mitandao ya kijamii kama
blogs kama vyombo vya habari ambapo TCRA inaandaa utaratibu kukutana na
wamiliki na waandishi wake kujadili juu
ya matumizi mazuri vyombo hivyo vya mawasiliano.
Mkurugenzi huyo amesema kwa
kushirikiana na TCRA watashauriana jinsi ya kutafuta wataalamu kwa ajili ya kutoa mafunzo
mbalimbali juu ya matumizi ya mitandao na ujuzi zaidi katika mawasiliano ya
mitandao husika.
Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika kutumia vyombo vya
mawasiliano kwani kutumia mawasiliano
vibaya ni makosa kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya
kielectroniki na posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Profesa Nkoma
amewataka watumiaji wote wa simu za mkononi na wananchi wote kuunga
mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kuharakisha
maendeleo ya sekta ya mawasiliano ambayo huchangia uchumi wa taifa na kuiweka
Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano wanaarifiwa kuwa
wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki watoe taarifa kwa vyombo husika, kisha
waufute ujumbe huo kwani wakieneza kwa watu wengine watakuwa sehemu ya uhalifu.
0 comments :
Post a Comment