-->

TAMTHILIA YA KWELI KUHUSU WANAFUNZI WA KIISLAM WA MBEKENYERA HIGH SCHOOL

Wanafunzi wa wa kiislam wa shule ya sekondari Mbekenyera ya huko Lindi nchini Tanzania wamekumbana na madhira ya kukosa uhuru wao wa kiibada baada ya kunyang'anywa kila eneo ambalo wanalitumia kusalia au kuendeshea ibada zao.Tukio hilo la kutimuliwa katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyatumia kwa ibada limetafsiliwa kama kukataliwa kwa wanafunzi hao kuswali swala tano wakiwa hapoa shuleni,Kwani yasemekana kwamnba Mwl aliyefahamika kwa jina la Emmanuel P. Romano alitamka kwamba kwa yule aliyekuja kusoma basi na asome na sio kuswali.Kauli hiyo yasemekana kumtoka Mwl huyo wakati wa kadhia ya kuzuia kutumika kwa choo ambacho kilikuwa karibu na Chumba cha kusalia amabacho kilikuwa kama mskiti kwa wanafunzi hao kwani walipewa na mkuu wa shule ambaye alikweshapita.Pia katika kadhia hiyo ambayo ilipelekea baadhi ya wanafunzi hao takriban 9 kupigwa na kupelekwa polisi.Baadhi ya wanafunzi hao ni pamoja na Choni,Chacha na Njachama,kipindi kadhia hiyo ambayo ilileta tafrani ndani ya shule hiyo Amiri wa shule wa wanafunzi wa kiislam alikuwa ni Bakari Kigunguyu.
KWA HABARI ZAIDI KUHUSIANA NA KDHIA HII SOMA GAZETI LA ANNUR HILI HAPA CHINI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment