CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete
kuunda tume huru yenye nguvu ya kimahakama kwa ajili ya kuchunguza
vifo, mauaji na mateso yaliyowahi kufanywa na vyombo vya dola kwa raia
wasio na hatia badala ya kamati zisizo na manufaa.
Kauli hiyo ya chama hicho inatokana na tukio la kupigwa risasi kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kauli hiyo ya CHADEMA ilitolewa Jumanne wiki hii na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Profesa Abdallah Safari, wakati alipozungumza na wanahabari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Msomi huyo wa masuala ya sheria, alisema matukio ya watu kuuawa na kuteswa yamekuwa yakiongezeka na kauli ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa polisi wawapige wanaoleta vurugu, inaonyesha kuwa kuna mkono wa serikali kwenye matukio hayo.
“Hatuna imani na kamati iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la Ponda inayoongozwa na Isaya Mungulu. Huyu bwana ametumwa katika maeneo mengi kuchunguza matatizo na hadi sasa hakuna taarifa yoyote aliyowahi kuitoa.
“Iundwe tume huru ya kimahakama au kijaji kwa ajili ya kuchunguza vifo, mauaji na mateso yanayofanywa na vyombo vya dola. Matukio ya kuchunguzwa na tume hiyo ni kama mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi, mateso ya Absalom Kibanda, Mwembechai, Bulyanhulu, kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka na tukio la Arusha,” alisema.
Akizungumzia suala la Ponda, Safari aliweka wazi kuwa kwa utaalamu wake wa kisheria, Polisi walidhamiria kumuua Sheikh Ponda na wala si kumjeruhi ili kumkamata kwa urahisi.
“Nimesimamia kesi nyingi za mauaji, Sheikh Ponda amepigwa katika bega la kulia karibu na kifua kisheria mtu anapopiga maeneo ya kifua amedhamiria kuua, hiyo inakuwa ni kesi ya kuua na wala si kukusudia kuua ‘manslaughter’ laiti Sheikh Ponda angefariki basi polisi wangekuwa na kesi ya kujibu.
“Nilikuwa Morogoro wiki hii nimekutana na watu waliokuwepo kwenye eneo la tukio na hata ndugu yake Sheikh Ponda alipokuwa Muhimbili pale Taasisi ya Mifupa - MOI alizungumza wazi kuwa polisi walihusika kumjeruhi kwa risasi kiongozi huyo katika harakati za kutaka kumkamata,” alisema profesa huyo.
Aidha msomi huyo aliwaeleza wanahabari kuwa ushahidi uliotolewa na madaktari juu ya jeraha la Sheikh Ponda kutokuwa la risasi si wa kuzingatiwa sana kwani kisheria ushahidi wa kitaalamu ni ushahidi wa pili baada ya ule wa mtu aliyekuwepo eneo la tukio.
Alihoji kuwa kwanini serikali inang’ang’ania kuchukua ushahidi wa madaktari wakati Sheikh Ponda hakujeruhiwa chumbani. Wakati polisi wanafika eneo la mkutano kulikuwa na watu wengi sana wanatosha kuwa mashahidi.
“Wakati Jeshi la Polisi likijikanganya kwa kujaribu kuficha ukweli wa tuhuma zinalolikabili za kumpiga risasi kiongozi huyo wa dini, kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, RPC Faustine Shilogile amenukuliwa na vyombo vya habari vya nje ya nchi (Uingereza) akikiri kuwa jeshi hilo linahusika kumpiga risasi Sheikh Ponda katika harakati za kutaka kumkamata,” alisisitiza Profesa Safari.
Mbali na CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba kimelaani tukio hilo na kutaka kuitishwa kwa uchunguzi huru. Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) pia ni miongoni mwa taasisi zilizolaani tukio hilo na kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kujiuzulu ili kupisha uchunguzi huru wa tukio hilo.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/chadema-yajitosa-kwa-sheikh-ponda#sthash.nmpOpw7G.dpuf

0 comments :
Post a Comment