KATIBU
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda
(54), Leo jioni amesomewa shitaka la kuhamasisha wafuasi wake kufanya
kosa huku akiwa katika chumba cha Wagonjwa kwenye kitengo cha Taasisi ya
Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI).
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkazi Kisutu, Helen Riwa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, amesema uhamasishaji huo umefanyika sehemu mbali mbali nchini kuanzia Juni 2 mpaka Agosti 11 Mwaka huu. Kweka amesema kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu 390 na 35 ya kanuni za adhabu.
Kutokana na Shtaka hilo hakimu Riwa aliahirisha kesi hadi agosti 28 na kutoa agizo Sheikh Ponda aendelee kuwa chini ya uangalizi wa vyombo vya dola akiwa anaendelea kupata matibabu hospitalini hapo.
Baada ya hakimu Riwa kuahirisha kesi wakili wa Sheikh Ponda Nasoro Jumaa, alilaumu utaratibu uliotumika na kusema mahakama imefanya kazi nje ya muda wa kawaida wa saa za kazi za kiserikali. Alisema mawasiliano ya awali ni kwa askari pamoja na tume ya haki jinai ya jeshi la Polisi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya mahojiano na Sheikh Ponda.
Aliongeza kuwa baada ya maofisa hao kufika hali ya Sheikh Ponda haikuweza kuruhusu mahojiano kufanyika ambapo ilipofika saa kumi jioni kila mmoja alitawanyika. Wakili Jumaa alisema wakiwa wanakaribia geti la kutokea muhimbili walipigiwa simu kuwa Sheikh Ponda anasomewa mashtaka hali iliyowafanya washangae utaratibu huo wa serikali wa kufanya kazi kwa kuvizia.
Kama walikuwa na dhamira ya kumsomea mashtaka wangetuambia kwa kuwa ni haki ya msingi kwa mtuhumiwa kuwa na mwanasheria wake kwa ajili ya kujua taratibu zilizotumika” alisema Wakili Jumaa. Alisisitiza kuwa baada ya kupata hati ya Mashtaka wanajiandaa kupinga kosa hilo kwa kile alichoeleza kuwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu haina uwezo wa kusikiliza kosa la aina hiyo.
Aliongeza kuwa kabla ya kufikiwa kwa hatua ya kumsomea Shtaka Sheikh Ponda,walishaandika barua ya kutokuwa na imani na tume ya haki jinai ya Polisi katika uchunguzi wao kwa kile alichoeleza kuwa Polisi ndiyo watuhumiwa wa kwanza katika tukio la kujeruhiwa kwa mteja wake.
Awali kabla ya kesi hiyo kusomwa maeneo mbali mbali ya hospitali ya Muhimbili hususan jirani na jengo alilolazwa Sheikh Ponda, Makachero wa jeshi la Polisi walikuwa wametanda kila eneo huku kukiwa na magari matano ya kikosi cha kutuliza ghasia.
Magari mawili yenye namba PT 2072 na PT 2061 yalikuwa jirani na mlango wa kuingilia katika kitengo cha mifupa cha MOI.huku askari wa jeshi hilo wakiwazuia wananchi waliotaka kumuona Sheikh Ponda kwa kile walichoeleza kuwa kuna shughuli za kiserikali zinaendelea.
Miongoni mwa watu waliozuiwa kumuona Sheikh Ponda ni Pamoja na wakili Maarufu nchini Profesa Abdallah Safari.
- See more at: http://www.fikrapevu.com/sheikh-ponda-asomewa-mashtaka-hospitalini-muhimbili/#sthash.ZXmjuXcZ.dpuf

0 comments :
Post a Comment