Mwalim Mariam Khamisi Mhitimu wa chuo kikuu cha Waislam Morogoro ambae pia amekuwa mwalimu mkongwe katika shule ya Morogoro secondary amefariki dunia huko Dar es salaam katika hospitali ya Muhimbili wakati anapatiwa tiba ya kansa ya kizazi.Aidha marehemu kabla ya kufahamika kusumbuliwa na kansa ya kizazi alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Kwa mujibu wa ripota wetu Mwl Mariam Khamisi alilzwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam ambako umauti ulimkuta akiwa huko.
Mwalim Mariam Khamisi ni mhitimu wa chuo kikuu cha waislam Morogoro katika mwaka 2014 yaani alijiunga na chuo hicho mwaka 2011 na kuhitimu shahada yake mwaka 2014.
Mwl Mariam Khamisi atakumbukwa na wanafunzi wengi aliowafundisha akiwa Morogoro Secondary,pia wafanya kazi wenzake pamoja na walimu na wanafunzi wa chuo kikuu cha waislamu Morogoro.Ama kwa hakika ndugu jamaa na marafiki wamekumbwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na ndugu yao kipenzi.
Kwa taarifa zilizotufikia mazishi ya Mwalim Mariam Khamisi yatafanyika mkoani Morogoro katika wilaya ya Mvomero.
SISI SOTE NI WA MWENYEZIMUNGU NA KWAKE TUTAREJEA

Mwalim Mariam Khamisi katika zama za uhai wake
SISI SOTE NI WA MWENYEZIMUNGU NA KWAKE TUTAREJEA
0 comments :
Post a Comment