Mchezaji bora wa mechi, Kessy (kulia)
HASSAN
Ramadhan Kessy aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora Simba ikitinga nusu
fainali ya kombe la Mapinduzi kwa kuifunga mabao 4-0 Taifa ya Jang’ombe
katika kipute cha robo fainali kilichofanyika uwanja wa Amaan jana usiku
ameigomea zawadi hiyo.
Akizungumza
jana na mtandao huu dakika chache baada ya mechi kumalizika, Kessy
alimshukuru Mungu kwa kucheza vizuri na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora
wa mechi na kupewa zawadi ya King’amuzi cha Azam TV.Hata hivyo
beki huyo wa kulia aligoma kupewa hadhi ya kuwa mchezaji bora badala
yake alisema mfungaji wa mabao matatu katika ushindi wa Simba, Ibrahim
Hajibu ‘Mido’ ndiye alistahili kuwa mchezaji bora.
“Nimepewa
zawadi, nashukuru. Lakini sijui wametumia vigezo gani, mimi naona
Hajibu (Ibrahim) alistahili kuwa mchezaji bora”. Alisema Kessy.
Nyota
huyo aliyejiunga na Simba wakati wa dirisha dogo la usajili desemba
mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar alisema kikosi cha Simba kinazidi
kuimarika chini ya kocha mpya.
“Tunashukuru
Mungu tunacheza vizuri. Kocha amekuja na mbinu mpya. Mashabiki
‘waisapoti’ timu yao. Simba ni timu yetu sote, tukiwa na umoja tutafanya
vizuri”. Alisisitiza Kessy.
Dakika za lala salama katika mechi hiyo, Kessy alitolewa na nafasi yake ilichukuliwa na beki mkongwe, Masoud Nassor ‘Cholo’.
Simba
inasubiri mpinzani wake wa nusu fainali katika mechi ya mapema leo saa
9:00 alasiri baina ya mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda na
Polisi Zanzibar.
Mechi
nyingine ya robo fainali itaanza majira ya saa 11:00 jioni baina ya
Azam fc na Mtibwa Sugar, wakati saa 2:15 usiku katika uwanja huo wa
Amaan, Yanga watahitimisha hatua hiyo kwa kuchuana na JKU ya Zanzibar.
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment