KOCHA mpya wa Simba SC, Goran Kopunovic raia wa Serbia ameendeleza
wimbi la ushindi katika mechi ya sita mfululizo, baada ya kuiongoza
timu hiyo kupata ushindi wa mabao 20 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara jioni ya leo. Ushindi huo wa pili katika mechi tisa za
Ligi Kuu kwa Simba SC msimu huu, unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi
watimize pointi 12 na kufufua matumaini ya ubingwa. Hadi mapumziko,
tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 10 lililofungwa na mshambuliaji
Mganda, Dan Sserunkuma dakika ya 26 aliyemalizia kwa guu la kushoto kona
ya Ramadhani Singano ‘Messi’. Kipindi cha pili, Simba SC iliyotwaa
Kombe la Mapinduzi Zanzibar wiki iliyopita chini ya Kopunovic,
ilifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68 kupitia kwa Elias Maguri
aliyemalizia pasi ya Dan Sserunkuma.
Wakati huohuo UBUTU
wa safu ya ushambuliaji ya Yanga SC kwa mara nyingine umeendelea
kuitesa timu hiyo, baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bila
kufungana na Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara. Washambuliaji wa Yanga SC, Kpah Sherman, Amisi Tambwe,
Simon Msuva na Andrey Coutinho wote walikosa mabao ya wazi leo. Refa
Mohammed Theofil wa Morogoro aliyesaidiwa na Michael Mkongwa wa Njombe
na Yussuf Sekile wa Ruvuma, alilazimika mara kadhaa kuamulia ugomvi
baina ya wachezaji wa timu zote mbili.
KIKOSI CHA TIMU YA YANGA
AZAM yaibanjua Stendi
MABINGWA watetezi, Azam FC
wamefanikiwa kupata ushindi wa bao 10 dhidi ya wenyeji Stand United
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga. Shukrani kwake, kiungo aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu,
Frank Raymond Domayo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 43 na sasa Azam
FC inatimiza pointi 17 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi kwa
pointi moja Mtibwa Sugar iliyokuwa juu kwa muda mrefu. Azam FC ilicheza
vizuri na ingeweza kupata mabao zaidi kama washambuliaji wake wangetumia
vizuri nafasi walizotengeneza, wakati Stand United licha ya kucheza
nyumbani, hawakuwa tishio.
Azam Fc
0 comments :
Post a Comment