Mamba aonekana akiwa hai Kengeja Pemba
Katika hali isio ya kawaida wananchi wa kijiji cha Ukunda Mkumbi Kengeja wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba kwa mara ya kwanza wameshuhudia uwepo wa mamba ndani ya kijiji hicho huku akiwa hai.
Kuonekana kwa mamba huyo kumekuja baada ya baadhi ya watoto wa kijiji hicho walipokuwa wakivua samaki kwenye ziwa dogo ambalo lipo karibu na bahari kijijini hapo.
‘’Ni kawaida yetu sisi kuja kuvua samaki maneo haya kila tunapopata nafasi lakini leo tunashangaa baada ya kuvua samaki tunavua mamba huyu’’walisika watoto hao.
Huku hayo ya kijiri baadhi ya makundi ya watu wamekua wakifurika kumuona mamba huyo huku wakishangazwa mno kuona kiumbe hicho kwa mara ya kwanza.
Wakati makundi ya watu wakiendelea kufika eneo hilo kwa ajili ya kushuhudia kiumbe hicho baadhi yao wameiomba Serikali kupitia uongozi wa wilaya kufika eneo hilo ili waweze kutoa alau ufafanuzi juu ya kiumbe hicho kwa vile ni kiumbe cha maajabu kwao na hawajawahi hata kusikia uwepo wa viumbe hivo kwa Zanzibar.
Aidha wananchi hao kwa sasa wamefanya jitihada za kumchukua mamba huyo na kumueka eneo maalumu ambalo kuna mfereji wa maji huku wakisubiria uamuzi kutoka kwa Serikali husika nini wafanye kuhusu mnyama huyo.
Kwa upande wa Sheha wa Shehia hio ya kengeja Bwana Muhammed Kassim ambae alifika kwenye tukio hilo alithitisha kutokea kwa mamba huyo na kuwataka wananchi kutokua na hofu wakiamini ni jambo la kawaida linaloweza kutokea popote pale.

0 comments :
Post a Comment