Limao ni kitu kidogo sana lakini faida
zake huwezi kuamini kama hujawahi kutumia. Kuna faida nyingi sana za
kutumia limao, hasa wakati wa asubuhi wakati mwili umekaa bila kula
usiku kucha. Kati ya nyingi, hizi hapa chache za kukufanya kufikiria
kuanza kutumia limao kama utapenda.
Kusafisha mwili
Limao husaidia kusafisha uchafu usiohitajika mwilini kwa kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini kufanya kazi vizuri.
Kuweka harufu nzuri kinywani
Asidi iliyopo kwenye maji ya limao huua
bakteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ni
vizuri kama ukinywa limao baada ya kupiga mswaki ili kupata matokeo
mazuri zaidi.
Kuleta nguvu mwilini
Limao baada ya kuingia kwenye mfumo wa
chakula, huupa mwili nguvu. Hii husaidia kuondoa uchovu na msongo wa
mawazo, sonono (depression), na wasiwasi.
Kupunguza uzito
Nyuzinyuzi za pectin (Pectin fiber) zilizomo kwenye limao husaidia kuzuia njaa na hivyo kutopata hamu ya kula mara kwa mara.
Kuongeza kinga ya mwili
Malimao yana acid, ni chanzo kizuri cha
vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa. Malimao pia husaidia
kuimarisha ubongo na mishipa ya fahamu kutokana na kuwa na madini ya
Potassium. Vilevile Potassium husaidia kuzuia shinikizo la damu.
Kuzuia uvimbe
Cha kushangaza kabisa, ukiwa unakunywa
maji ya limao mara kwa mara, unapunguza kiwango cha acid mwilini mwako.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa limao haitengenezi acid mwilini baada ya
kumeng’enywa. Kutokana na hii, husaidia sana kupunguza asidi ya uric
ambayo ni chanzo kikuu cha uvimbe mwilini.
Kuondoa mikunjo na makovu mwilini
Maji ya limao huweza kuondoka makovu na
mikunjo kwenye ngozi. Huweza vilevile kupunguza makovu makubwa kama
ukinyunyizia kila mara. Kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji
ya limao huacha ngozi ikiwa inang’aa na yenye afya.
Husaidia kukufanya uache kunywa kahawa
Je wewe ni mlevi wa kahawa na unataka
njia ya kuacha ? Basi kunywa kikombe cha maji ya moto chenye
mchanganyiko wa limao. Hii ni dawa tosha. Huwezi kuamini hadi ujaribu,
na ukishajaribu hutoweza kurudi tena kwenye kahawa.
Je unatakiwa kutumia limao kwa kiwango gani?
Kama una uzito mdogo, chini ya kilo 70,
unaweza kula nusu limao, kama umezidi kilo 70 unatakiwa kula limao zima
kwa siku. Ukifanya hivi kila siku utaanza kuona mabadiliko muda si mrefu
0 comments :
Post a Comment