-->

GERVINHO AOMBA RADHI KWA KADI NYEKUNDU ALIYOIPATA

GERVINHO AOMBA RADHI
Mshambuliaji wa Ivory Coast Gervinho ameomba radhi baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumshambulia beki wa Guinea Naby Keita, katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 siku ya Jumanne.
"Nataka kuomba radhi kwa taifa la Ivory Coast, wachezaji wenzangu, mashabiki na waandalizi wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa jambo lile la hasira," ameandika kupitia Twitter.
"Sio kawaida yangu, na jambo hilo halina nafasi uwanjani."
Kadi nyekundu ya kosa la ushari adhabu yake ni kukosa mechi zisizopungua mbili, lakini katika Kombe la Mataifa adhabu inaweza kufika hata mechi nne iwapo kamati ya nidhamu itahisi adhabu zaidi inatakiwa.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal alionekana kama akimzaba kibao Keita katika dakika ya 58 katika mechi ya kundi D iliyochezwa Malabo.
Ivory Coast walikuwa wamefungwa goli moja tayari wakati huo, lakini waliweza kusawazisha, licha ya kuwa na mchezaji pungufu.
Gervinho, 27 alikuwa chachu katika mechi hiyo na iwapo atapewa adhabu na kukosa mechi mbili dhidi ya Mali na Cameroon litakuwa pigo kubwa.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment