Askari
jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka
watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana
miongoni mwa mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi
mbili hizo.Na inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji
wa tukio hilo.
Boko
Haram siku za hivi karibuni zimekamata udhibiti wa miji kadhaa na
vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na sasa wameanza kuwa
tishio kwa nchi jirani wanazopakana na Nigeria .Katika shambulio hilo la
siku ya Jumapili askari hao walivamia vijiji viwili vilivyoko eneo la
Tourou .
Katika
uvamizi huo nyumba kadhaa zilichomwa moto na idadi ya mateka ni
themanini kati yao watu wazima ni thelathini,na watoto wapatao hamsini
na walielekea upande wa Kaskazini mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo.
Cameroon imekuwa ikiishutumu Nigeria kwa kushindwa kufanya juhudi za ziada za kukabiliana na kundi hilo la Boko Haram.
0 comments :
Post a Comment