"Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika
maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi
wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content).
Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. Ninajua nchi yetu
inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala
ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua 'transformation'
inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa
nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua
rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha
maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na
kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi,
Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu"
Chambi Chachage kanikumbusha maneno yangu haya. Nimesisimka
0 comments :
Post a Comment