Licha ya upinzani mkali dhidi ya mswada wa marekebisho ya sheria za usalama, hatimaye rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta ametia saini mswada huo na kuwa sheria. Kwa haya, Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki ingependa kutaja yafuatayo:-
Kupitishwa kwa haraka na kimabavu kwa kanuni hii nikuonesha nia mbovu ya serikali na vikosi vyake vya Usalama ya kuendeleza ukatili na maonevu kwa raia wake na hasa Waislamu ambao moja kwa moja ndio walengwa kwenye vita dhidi ya Ugaidi. Twasema; ni kuendeleza kwani hata kabla ya kupitishwa mswada huu tayari jamii ya Kiislamu imeshuhudia mauaji yaliyofanywa na vikosi vya usalama kwa tuhuma za ugaidi.
Inaonekana kuwa kanuni hii ya kidhulma itafanya vita dhidi ya ugaidi kuchukua mkondo mpya, nao ni kunyamazishwa vyombo vya habari visiweze kufichua ukatili na mateso yatakayofanywa na vikosi vya usalama! La kusikitisha ni kuwa licha ya polisi kuhusika na mauaji kama inavyobainishwa na vyombo vya habari serikali hukana ukatili huo! Kanuni hii inaendelea kufichua zaidi urongo wa siasa ya kidemokrasia na miito yake ya uhuru ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari. Huku wanasiasa wakidemokrasia wakila viapo vya kutetea na kanuni zake wakati huo huo wanazipiga mateke na kuja na kanuni nyengine ambazo zenyewe zagongana na katiba zao. Ni hivi karibuni tu ilibainika rasmi huko Marekani taifa linalojigamba kote dunia kuwa mtetezi wa haki za kibinadamu jinsi maofisaa wa shirika la Kijasusi la CIA walivyohusika na matendo ya kikatili dhidi ya washukiwa wa kigaidi. Kwa kifupi mfumo wa kibepari ni urongo kiasi kuwe wenye mabepari hawauamini.
Usalama hauimarishwi kwa kupitishwa kanuni za kinyama ambazo zenyewe zinahujumu usalama. Tumekuwa tukikariri kuwa vyombo vya usalama ndani ya nchi za kidemokrasia hutumiwa na wana-siasa katika kulinda tu maslahi ya wanasiasa wala sio raia. Wanasiasa wafisadi huhonga polisi ile kuendeleza maovu yao kwa raia. Ni mara ngapi walanguzi wa madawa ya kulevya hushirikiana na vikosi vya usalama kwenye biashara hii fisidifu.
Mwisho tunaamini kuwa kanuni zote za kupambana na ugaidi zina mkono wa wamagharibi ndani yake. Na kama tulivyosema ni kuwa wamagharibi wameshindwa kukabiliana na Uislamu kifikra na sasa wanatumia mabavu dhidi ya mfumo wa haki wa Uislamu ambao hivi karibuni dola yake ya Khilafah itasimama na kuongoza ulimwengu kwa sheria za haki na uadilifu.
KUMB: 06 / 1436 AH Jumapili 29 Swafar 1436 AH 21/12/2014 CE
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki
Tel.: +254 720597841 / +254 789 574 608
Email: media@hizb-eastafrica.com
Hizb ut Tahrir Official Website
www.hizb-ut-tahrir.org
www.hizb-ut-tahrir.org
Hizb ut Tahrir Media Office Website
www.hizb-ut-tahrir.info
www.hizb-ut-tahrir.info
SOURCE:HIZ TAHRIR
0 comments :
Post a Comment