-->

PAPA FRANCISCO:SHOGA SIO TATIZO,TATIZO KAMPENI ZA USHOGA

 Papa Francisco.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amesema hawezi kuwahukumu mashoga, lakini akalaani kampeni ya kuhalalisha ushoga akiiita tatizo kubwa. Vile vile Papa Francis amesema kanisa halina budi kuwapa wanawake majukumu makubwa, ingawa amesema kuwa milango ya wao kuwa mapadre imefungwa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege yake akitokea Brazil kurudi Roma, Papa Francis alisema kuwa shoga sio tatizo, tatizo kampeni ya kuuhalilisha. Alisema kama mtu ni shoga na anamtafuta mungu kwa nia ya dhati, basi yeye hawezi kumhuku.
Kiongozi huyo wa wakatoliki ulimwenguni alijibu maswali kuhusu mtu aliyemteuwa kuongoza banki ya Vatican yenye matatizo, Battista Ricca, ambaye licha ya uteuzi huo anasakamwa na shutuma ya kuwa na uhusiano wa kingono na shoga. Papa amesema aliagiza uchunguzi mfupi juu ya madai hayo, lakini hakukua na ushahidi wowote dhidi ya mtu huyo.

Tarehe 11 mwezi july Mwaka 1976 mashoga wakiandamana kudai haki zaokuai haki zao za ushoga
File:Gay Rights demonstration, NYC 1976.jpgHABARI NA DW SWAHILI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment