Kwa wiki kadhaa zilizopita kumekuwepo na taarifa nyingi zinazomuhusu beki
wa kimataifa wa Tanzania na timu ya Simba, Shomari Kapombe kwamba
anatarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni kwenda nchini Uholanzi kwa
ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Twente.
Kapombe
ambaye mwaka jana alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa Tanzania amekuwa
na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na Simba akitokea Polisi Morogoro
miaka mitatu iliyopita kwa kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Karibia
vyombo vya habari vyote nchini vimekuwa vikikaririwa kwamba Shomari
Kapombe anatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya FC Twente,
ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi katika msimu wa 2009-10,
pia ilifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
katika msimu huo.
Kwa upande wa viongozi wa Simba mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed Nkwabi alikaririwa na gazeti la Mwananchi akisema
kwamba,”timu atakayokwenda kufanya majaribio Kapombe huko nchini
Uholanzi ni FC Twente, suala la ataondoka lini kwenda kufanya majaribio
tutawaambia safari itakapokuwa tayari.”
Na kwa upande wa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alikaririwa akizungumza kwenye kipindi cha michezo cha Spoti Leo cha
Radio One akisema kwamba amekwishatoa kibali kwa Kapombe kuondoka
nchini siku yoyote kuanzia sasa kwa ajili ya kufanya majaribio nchini
Uholanzi.
Lakini
baada ya kuwepo kwa taarifa hizi mtandao huu ulijaribu kufanya utafiti
kidogo kuhusu suala la usajili wa mchezaji huyu kwenda FC Twente na
kugundua vitu kadhaa vya utata kuhusu ukweli wa taarifa za Kapombe
kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi.
UKWELI
Mtandao feki |
1:
Kwanza kabisa chanzo kikuu cha taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente
zilizotolewa na mtandao wa www.fctwente.nu - ambao sio mtandao rasmi wa
klabu ya FC Twente.
Kwa
mujibu wa mtandao rasmi wa klabu ya FC Twente anuani yake ni hii
(http://www.fctwente.nl/en/). Mtandao huu rasmi wa klabu hii haukuwa na
taarifa zozote kumuhusu Shomari Kapombe au mchezaji mwingine wa Simba na
Tanzania kiujumla.
2:
Katika kupata uhakika zaidi mtandao huu ulijaribu kuwasiliana na afisa
habari wa klabu ya FC Twente, Bwana Richard Peters kuhusu ukweli wa
klabu yake kumtaka Shomari Kapombe kutoka Tanzania. Lakini afisa habari
huyo alikanusha taarifa hizo na akisema kwamba klabu yake haina taarifa
zozote kuhusiana na mchezaji huyu Kapombe. Akisisitiza kwamba mtandao
ulioripoti taarifa za usajili wa Kapombe sio sahihi na zimetolewa na
mtandao usio rasmi.
3:
Mtandao huu haukuishia hapo, tulijaribu kumtafuta wakala
anayeshughulikia kumtafutia Kapombe timu nje ya Tanzania, Bwana Denis
Kadito ambaye alithibitisha ni ukweli kwamba alikuwa katika mpango wa
kumpeleka Kapombe Uholanzi ili aanze kumtafutia timu ndani ya bara la
ulaya, na alipoulizwa kuhusu taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente,
Dennis alisema hana taarifa zozote za Kapombe kutakiwa na FC Twente
hivyo hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.
SOURCE:SHAFFIH DAUDA
0 comments :
Post a Comment