-->

LITA 600 YA POMBE HARAMU YAKAMTWA DODOMA

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limefanikiwa kukamata lita mia sita (600) za pombe haramu ya Gongo, mitambo 11 pamoja na mapipa 134 ya (molasisi) ambayo ni mali ghafi inayotumika kutengenezea pombe hiyo.

Mafanikio hayo yametokana na operesheni maalumu ya msako iliyofanyika tarehe 27/07/2013 katika wilaya Kongwa, Kijiji cha Kimero –Kiteto Kata ya Lenjulu Tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa.

Pia tumefanikiwa kukamata debe kumi za Bhangi, ambazo zimekamatwa huko katika kijiji cha Garigari kitongoji cha Mfiro wilayani Mpwapwa, ambapo debe nane zimeteketezwa.

Aliyekamatwa na pombe ya gongo, mitambo 11 na mapipa 134 ya molasisi ni TAITA S/O MASHAKA RASHIDI@Rashid, Mchaga,miaka 40, mkulima na mkazi wa Kimero Kiteto Kongwa.

Waliokamatwa na Bhangi huko Mpwapwa ni;
1. FREDRICK S/O NGIMBA, Mhehe, miaka 25,mkulima,
2. EMANUEL S/O NGIMBA, Mhehe, miaka 28,mkulima,
3. JUMA S/O NGIMBA, mhehe,miaka 46, mkulima wote wakazi wa kijiji cha Garigari.

Tunashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kutupa taarifa zinazoleta mafanikio kama haya ya kupungufa uhalifu na madhara kwa afya za watu.

DAVID A. MISIME- ACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment