-->

ROBERTO MARTINEZ AWA MRITHI WA DAVID MOYES EVERTON

RM

 

Everton Wamemteua kocha wa Mabingwa wa kombe la FA Wigan Athletic, Roberto Martinez kama kocha mkuu wa timu hiyo katika mkataba wa miaka minne akirithi mikoba ya David Moyes aliyetimkia Man United.

Martinez ambaye ni raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 39 ameisaidia Wigan kushinda kombe la FA msimu huu japokua aliombwa kuiacha Wigan baada ya kushindwa kuiokoa kushuka daraja anarithi mikoba ya David Moyes aliyejiunga na Manchester United kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Sir Alex Ferguson.


Uongozi wa Wigan ulisema " Mchango wa Roberto katika klabu akiwa kama mchezaji na hatimaye kocha wa Wigan kwa muongo mzima utakumbukwa milele na mashabiki wote wa Wigan".

Martinez ameichezea Wigan michezo 180 kama mchezaji kati ya mwaka 1995 na 2001 kabla hajarudi klabuni hapo kama kocha miaka 8 baadaye.

Chini ya Martinez, Wigan ilimaliza nafasi ya 16 mara mbili na nafasi ya 15 msimu uliopita kabla ya kushuka rasmi daraja msimu huu ikiwa katika nafasi ya 18.

Mwezi Juni 2011 alikua kati ya makocha waliopewa nafasi kubwa kuifundisha Aston Villa na kutokana na mapenzi yake aliamua kubaki uwanja wa DW na pia alihusishwa na kuchukua mikoba ya Liverpool msimu uliopita.

Martinez alijiunga na Wigan baada ya kuipandisha Swansea City kutoka ligi daraja la kwanza mpaka hatua ya Championship na kudumu na Wigan kwa misimu minne akiwa na kikosi kinachozinduka dakika za lala salama za ligi.

Mwenyekiti wa Wigan Dave Whelan alisema Jumatatu wiki hii kwamba wamekubaliana na mwenyekiti wa Everton  Bill Kenwright kumruhusu Martinez kuihama Wigan.


Martinez anachukua nafasi ya kuifundisha Everton iliyomaliza katika nafasi ya 6 msimu huu katika ligi kuu huku ikiwa ni mara ya 7 mfululizo Everton ikimaliza katika nafasi 8 za juu chini ya Moyes.


MAMBO MUHIMU KUHUSU ROBERTO MARTINEZ

  • Umri : miaka 39
  • Timu alizochezea : Real Zaragoza (1993-1994), Balaquer (1994-1995), Wigan Athletic (1995-2001), Motherwell (2001-2002), Walsall (2002-2003),Swansea (2003-2006), Chester City (2006-2007)
  • Timu alizozifundisha: Swansea (2007-2009) na Wigan (2009-2013)
  • Mafanikio kama Kocha: Bingwa ligi daraja la kwanza England (2007-2008), Kombe la FA (2012-2013)

SOURCE:wapenda soka
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment