MNYATE |
Kuna
taarifa za uhakika kwamba Simba imefanikisha usajili wa mshambuliaji wa
Mwadui FC, Jamal Mnyate kwa dau la Sh milioni 15 tu.
Mnyate
ndiye aliyeitoa Simba kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana
na bao lake alilowafunga kwenye mechi ya raundi ya pili kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam. Mwadui ilishinda bao 1-0.
Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza mshambuliaji
huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa dau hilo la usajili akiwa
kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba Mwadui.
“Mnyate
tumemalizana naye kama wiki moja iliyopita, amesaini mkataba wa miaka
miwili ya kuichezea Simba kwa dau la Sh milioni 15.
“Tulimsajili
kama mchezaji huru kutoka Mwadui FC mara baada ya mkataba wake
kumalizika wa kuichezea timu hiyo,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa
mshambuliaji huyo kuzungumzia usajili wake, alikiri kusaini Simba huku
akigoma kukubali au kukataa kuhusu dau la usajili.
“Siwezi
kutaja kiasi nilichosainia Simba kwani fedha ya usajili ni siri kati
yangu na klabu, hivyo siwezi kuzungumzia hilo,” alisema Mnyate.
SOURCE:SALEHE JEMBE
0 comments :
Post a Comment