-->

TSHABALALA KUBADILI JINA NA KUITWA ZIMBWE JR

Mchezaji Mohamed Hussein 'Tshabalala' aamua kubadili jina na sasa jezi yake kuwa na jina la ZIMBWE Jr.
Akiongea na Simba News kupitia simu alieleza sababu za kuachana na jina la Tshabalala ni kuwa halikuwa jina lake halisi bali la mchezaji wa zamani wa nchini Afrika Kusini Lawrence Siphiwe Tshabalala ambaye alitokea kumpenda jinsi anavyokuwa akicheza.
'Nimekuwa sijisikii vizuri pindi watu wakiniita jina la Tshabalala kwani si jina langu halisi, na ndio sababu iliyopelekea kuamua kutumia jina la kwetu kabisa, Zimbwe ni jina la mjomba wangu ambaye kwa sasa ni marehemu alikuuwa akiitwa Said Zimbwe' 'alimalizia Mohamed Hussein ' Zimbwe Jr'
 
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment