Siku chache kupita baada ya Mkutano
wa 19 wa Bunge kumalizika,na serikali kuutupia mbali mswaada wa sheria
ambao unaruhusu kuwepo makakama ya Kadhi nchini kutajadiliwa kwenye mkutano
huo,
Nayo Jumuiya na Taasisi za Kiislam
nchini wameibuka na kutoa tamko zito kwa kuwataka waislam wote nchini
kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba pendekezwa Bunge Maalum la
Katiba,kwa madai kwamba serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo
chake cha kukataa kuwepo mahakama ya Kadhi nchini.
Vilevile Taasisi hiyo imewataka pia waislam
wote kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura na kujiandaa
kufanya uamuzi mgumu ambao wanasema hajawai fanywa na waislam nchini tangu
taifa kupata Uhuru.
Akisoma Tamko hilo lenye kura
sita jana jioni kwenye msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Jijini Dar
es Salaam ,Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam nchini Sheikh
Mussa Kundesha kwa niaba ya asasi za kiislam 11 zinazounda umoja huo na kushuhudiwa
na Mamia ya waumini wa dini hiyo pamoja waandishi wa Habari ambapo Sheikh
Kundesha alisema.
Waislam wote nchini wamechoka na
uonevu wanaodai kufanyiwa na Serikali iliyoko madarakani kwa kitendo cha kuondo
Mswaada wa Mahakama ya kadhi Bungeni ambapo alisema ni kuendelea kuchochea vita
ya kidini nchini.
“Kuna kila sababu ya kuamini kuwa
Serikali ya CCM imeshindwa kulishughulikia suala la mahakama ya Kadhi katika
uhalisia wake kama ilivyoahidi kupitia ilani yake kwenye uchaguzi ibara ya 108
(b) mwaka 2005 na sasa inafanya hadaa za kisiasa kuwadanganya waislam ili
waonekane inalishughulikia suala la mahakama ya Kadhi kama walivyoahidi”
“Kwa ubabe huu wanaotufanyia waislam
sasa tunawaomba waumini wote wa kiislam nchini kutoipigia kura katiba
pendekezwa kwasababu sio katiba nzuri kwa waislam harafu tunawataka kila mmoja
aliyetimiza miaka 18 ajiandikishe kwenye Daftari wa wapiga kura kujiandaa
kufanya uamuzi mgumu ambapo utalitikisa nchi”alisema Sheikh Kundesha.
Alisema kuwa kitendo cha Serikali
kuwatambua Makadhi wa Bakwata pamoja wanachosema ni ‘Mahakama hewa ya Kadhi’
chini ya Bakwata ni kinyume na Katiba ya nchini ibara 19(1) na (20) kwa
kuwalazimisha waislam wawe chini ya Bakwata ambapo wanasema hawatakubaliana
nalo.
KUHUSU TAMKO LA MAASKOFU.
Pia katika Tamko la Taasisi
hiyo kiislam ambapo litasomwa kila msikiti Ijumaa wiki hii nchi nzima pia
wamezungumzia Matamko mawili yaliyotolewa Jukwaa la kikiristo nchini ambapo
Taasisi hiyo ya Kiislam wameonyesha masikitiko yao kwa kusema ni dhahili hapa
nchini kuna serikali dhaifu kwa kuwaacha maaskofu kutoa matamko ambayo wanadai
ni ya kichochezi.
“Ushahidi kwamba ni chuki tu husda
ni pale ambapo hata waislam tuliopendekeza mahakama ya Kadi iwekwe kwenye
Katiba pendekezwa,lakini tunashangaa hawa maaskofu wamekuwa wakiipinga Mahakama
hii wakati hii dini tofauti na y a kwao na sisi waislam tumewavumilia lakini
tunahoji hawa maaskofu wanataka nini”
KUHUSU KESI ZA MASHEIKH NA KUNYIMWA
DHAMANA.
Pia Taasisi ya Kiislam wameonyesha
kuchukizwa kwa kitendo cha Masheikh mbalimbali akiwemo shehe Ponda ambao wapo
mahabusu na kunyimwa Dhamana na Serikali ila wanashangaa kitendo cha Serikali
kuwamwachia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima wanadai
kitendo hicho kinaonesha Serikali kuwapendelea wakristo.
“Masheikh mbalimbali wako mahabusu
wakinyimwa Dhamana bila sababu za msingi kwa kesi za uchochezi au kwa
kisingizio cha Ugaidi wakati huo huo tumeshuhudia Maaskofu wakitoa kauli za
uchochezi pasina kuchukuliwa hatua yeyote ikiwemo sakata la Askofu Gwajima”
KAMPENI WANAO DAI KUUA MADRASA.
Pia Taasisi hiyo wamezungumia
kitendo cha Serikali kuwakamata wa Mashehe mbalimbali wanaowafundisha watoto
majumbani kwa madai ya serikali kutofuata taratibu za mafunzo likiwemo matukioa
tofauti yaliyotokea mkoani arusha-
Kwa kusema ni wazi serikali
imejitosa kuua madrasa nchini.
“Lakini Takriban mwezi mmoja
sasa,njama hizi za kuua madrasa zetu zimeibuka kwa kasi kubwa na nguvu kwa
kuendesha kamatakamata ya waalimu wa madrasa zao katika hali duni majumbani
mwao wakifundisha Quran na mafunzo mengine ya Uislam kama tulivyoshudia huko
mkoan Moshi na Arusha”
“Tunataka Serikali itusaidie
kufundisha Elimu ya dini ya Kiislam kwa mujibu wa sheria ndiyo ipi,sheria hiyo
ilipitishwa lini na Bunge lipi?kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara 20 (1) kazi
ya kutangaza dini ni suala binafsi,iweje sasa Serikali inakuja na madai haya ya
kufundisha dini kinyume na Sheria kwa walimu wetu wa madrasa”
SOURCE:MAKAMBAKO KWETU
0 comments :
Post a Comment