Hatimae viongozi wa chuo cha dini cha Al-jazeera(Markaz) wazungumza na vyombo vya habari mbali mbali na kukanusha madai yaliyo andikwa na mwandishi wa habari la gazeti la MTANZANIA ambae amefahamika kama Ratifa.Ratifa mwandishi wa habari wa gazeti hilo la MTANZANIA ameandika kwamba chuo hichi kilichopo Ukerewe kwamba kinajishughulisha na maswala ya kigaidi,Pia amesema kwamba chuo hicho huwa kinaingiza makontena ya silaha kupitia njia ambayo si halali,Pia ameongeza kwamba chuo hicho kinawanafunzi 600 katika hao kuna mchanganyiko wa watoto na wakubwa,ameeleza kwamba kuna watoto mpaka wa miaka kumi pamoja na watu wazima ambao hujishughulisha na mazoezi ya karate,kun fu pamoja judo.
Ama katika nyakati nyingine tofauti viongozi wa chuo hicho cha Ukerewe wamezungumza na vyombo vya habari na kukanusha madai hayo kwa kusema kwamba"chuo chetu hakijihusishi na mambo ya ugaidi na mambo yaliyoandikwa na gazeti la MTANZANIA hayana ukweli hata kidogo,hata ramani iliyo chorwa na gazeti hilo la MTANZANIA haiwiani na kabisa na ramani ya chuo hicho"Pia akapinga idadi ya wanafunzi iliyoandikwa na gazeti kwa kusema kwamba wanafunzi idadi yao haijafikia 600 bali inaangukia kwenye mia moja na ushee,Ramadhani Mazige akiongea kwenye kipindi cha Amplifaya cha tarehe 25mwezi wa pili katika radio ya CLOUDS FM.
Pia shekh Jabir kupitia gazeti la ANNUR la tarehe 1 ya mwezi wa tatu amebainisha kwamba hoja zilizotolewa na mwandishi wa gazeti la MTANZANIA ni hoja za kiftna na wala hazina mantiki kwa mwenye akili akitolea mfano swala la kuingizwa makontena kupitia mitumbwi.Pia alizungumzia swala la mafunzo ya karate,kun fu pamoja na judo kwamba mafunzo hayo hayatolewi chuoni hapo na hata kama yangekuwa yanatolewa hayawezi kumaanisha ugaidi kama ilivyoandikwa na gazeti hilo la MTANZANIA.Pia alibainisha hatua ambazo chuo hicho imezichukua baada ya kashfa ambayo imekichafua chuo hiko kwamba wameiandikia barua gazeti la MTANZANIA kwamba liandike taarifa nyingine ambayo itakanusha madai hayo na pia watatakiwa kulipa faini ya shilingi bilioni mbili kwa kitendo chao cha kukichafua chuo hicho ambacho kina baraka za mskiti pamoja na serikali(chuo halali kilichosajiliwa)
Ukurasa wa mbele wa gazeti la MTANZANIA kikiwa na kichwa cha habari kinachoashiria kuwepo kwa hofu ya kuwepo kwa ugaidi ndani ya chuo hicho
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment