-->

JE KADI NYEKUNDU YA NANI NI HALALI?

Katika mchezo wa kurudiana uliowakutanisha Manchester united na Real madrid refa wa mchezo huo alitoa kadi nyekundu ambayo iliibua mshangao katika macho ya watu wengi waliopo uwanjani hapo kwani hata wachezaji wa Real madrid hakuna hata mmoja ambaye alimkimbilia refa kumshinikiza kwamba mchezaji mwenzao kachezewa rafu mbaya.Lakini muamuzi alichukua maamuzi hayo makali dhidi ya mchezaji wa kireno Luis nani,kadi ilipekea taswira ya mchezo kubadilika na matokeo kuisha kwa 1-2 hali iliyompelekea kocha wa Manchester united kukasirika na kugomea kufanya mazunguzo na waandishi wa habari kama vile alivyotakiwa baadala yake alikwenda msaidizi wake Phelan.
Wadau wa soka wengi kama nile Gary Nevile wameipinga kadi nyekundu hiyo na kusema kwamba Nani hakudhamilia kucheza rafu kwani alisharuka juu kuufuata mpira kisha ndipo Abeloa alipotokea kwa nyuma na kutaka kuucheza mpira ule ule.pia alinukuliwa akisema
""Nani is a player who regularly tries to control a pass like this over his shoulder and its never a red card! Changed the whole game!Poor ref."
"Nani ni mchezaji ambae mara kwa mara huumiliki mpira katika namnahii kutoka kwenye mabega na haijawahi kuwa kadi nyekundu!amebadilisha mchezo mzima!Refa mbovu"
.hivyo kwa mujibu wa wadau wa soka wanasema kweli ilikuwa ni rafu lakini haikustahiki kadi nyekundu.Pia wamefananisha tukio kama hilo ambalo limefanywa na Luis Nani na matukio mengine ambayo maamuzi yake yalikuwa ni kadi ya njano
hiyo ni moja ya picha ambayo imeyakusanya matukio baadhi yanayofanana pamoja na adhabu ilyotolewa kama inavyoonekana kwa juu huku kwa chini ikiwa na maneno ya dhihaka dhidi ya maamuzi yaliyochukuliwa na refa huyo.
Pia UEFA wamekuja na maamuzi mapya huku yakiambatana na kusifia maamuzi ya refa kwamba ni sahihi na pia Manchester united wanajukumu la kuwajibika kutokana na utovu wa nidhamu uliofanywa na Rio Feedinand baada ya mechi kuisha kwa kumpigia makofi refa maskioni kwa alichowafanyia.UEFA wametafasiri kitendo hicho kama utovu wa nidham.
picha ya Rio Ferdinand akimpigia refa makofi ya dhihaka baada ya mechi kumalizika


Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment