Baada ya kuandika habari ya mbinu mpya ya utapeli wa kimtandao watu wengi huenda wakawa na shauku ya kutaka kujua kwamba je kuna ushahidi wowote kwamba TANZANIA LOANS SOCIETY ni matapeli?Ndio ushahidi umepatika katika wall ya Ridhiwani Kikwete akikanusha kwamba hakuna organisation ya ain hiyo kwa hapa nchini hivyo hao ni matapeli wa katika matandao.hapo chini ni nukuu ya habari aliyoiandika Ridhiwani Kkwete kwenye ukurasa wake wa facebook.
TAARIFA KWA UMMA JUU YA TANZANIA LOAN SOCIETY
Habari zenu mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale
wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo
soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .
Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi
kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo
yangu yatanyooka. Hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika
ufanikiwe lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu,
kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya
dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.
Hivi karibuni nimekuwa
napokea sana emails, sms, na hata tweets juu ya kitu kinachoitwa
TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana
kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Rais Barack Obama kuja
Tanzania kupitia Rais Dr. Jakaya Kikwete na sasa mimi nikishirikiana na
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha, jambo ambalo si la
ukweli hata kidogo na naomba kutumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele
ya umma wa Watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine
wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.
Kwa masikitiko
makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na
kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi
atakuwa AMETAPELIWA.
Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na
vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao
maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali
ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA
LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA
KIPATO KISICHO HALALI.
Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana
wenzangu ambao ninaamini kuwa muliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha
kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa
kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.
Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa
wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa
maneno na pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine
wameathiriwa na jambo hili. Haikuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea
ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima
ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza kufanya jambo
kumbe ndiyo unalikuza. Nniwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine
kurasa zao za Face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli.
MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment