-->

AJALI YA FIKRA NA TAIFA LA TANZANIA

Ajali imekuwa ni kitu kibaya na hakuna anaeombea ajali itokee katika mazingira yoyote kwani hupelekea watu kupoteza wanaowapenda au kuwafanya watu vilema wa kudumu katika maisha yao.Katika hali yoyote ile ajali haina faida isipokuwa ni athari kubwa huivaa jamii husika.
Tanzania ikiwa ni moja kati ya mataifa yaliyowahi kutawaliwa na mkoloni wakiingereza na kijerumani na kubahatika kupata uhuru wake ambao umekuewa ukitazamwa kama uhuru bendera kutokana na wananchi kutokuwa huru kiuchumi huku shida na matatizo zikiwa ndio rafiki wa karibu wa taifa la Tanzania toka lilipopata uhuru.Ukoloni kiujumla haukuishia kuyon7a mali ya taifa la Tanzania na kuitawala nchi hii ya Tanzania bali pia imesababisha AJALI KUBWA YA KIFIKRA,Kwa kutumia mifano ifuatayo msomaji unaweza pata taswira ya nini namaanisha;
GOLI LA KIZUNGU
Katika hali myingi sana za maisha ya mtanzania wamekuwa wakisifu vitu vizuri kwa kuumbatanisha na MZUNGU,Leo hii goli la kisigino limekuwa likiitwa goli la kizungu,Je magoli mengine ni ya kiafrika?kwa nini mzungu??Unaweza ukaona kawaida na ukajihisi wewe si miongoni mwa waliokumbwa na ajali ya kifikra,je ushawahi kujiuliza kwa nini vitu vizuri viambatanishwe na uzungu.
 MATANGO YA KIZUNGU
Matango makubwa ambayo ukiyaona kwa mara ya kwanza kama uliyazoea yale madogo huenda ukayashangaa kwani ni makubwa sana kupita kiasi kwa haya matango ni makubwa basi watu wengi nchini Tanzania huyaita matango ya kizungu.Yaani kila kinachoonekana kinastaajabisha uambatanishwa na Uzungu
VIAZI ULAYA
Viazi mbatata vimepeawa jina la viazi Ulaya kutokana tu na ubora wake kwani hutumika kupikia chips ambazo mara nyingi hupatikana kwenye vioski na mahoteli au kwenye mabar,viazi vile vingine ambavyo havitumiki kwenye kupikia chips ambavyo vinaitwa viazi vitamu wala hakuna mtu mwenye muda wa kuviita viazi hivyo viazi ulaya.
KAMA MZUNGU
Kiukweli inashanagaza sana hasa kwa mtu mwenye kufikiri kwani lazima ujiulize ukila vizuri watu wanakwambia unakula kama mzungu,ukitembea vizuri pia unajinadi kwamba unatembea kama mzungu,ukigundua kitu kizuri pia unajisifu kwamba umefanya kama mzungu..hii ni ajali ya fikra ambayo athari haitizamwi kwa undani ntaieleza wakati naitimisha
BORA KUWA MBWA ULAYA KULIKO KUWA RAIA TANZANIA
Leo hii vijana wamefika hatua ya kutamani na kupenda kuwa Mbwa Ulaya kuliko kuwa binaadamu Tanzania,hii ni zao la ajali ya kifkra yoyote utakaemskia akisema hivyo basi tambua huyo ni muhanga wa ajali ya kifkra...inaskitisha kuona hata wasanii wa Tanzania nao wanaimba kwamba bora wawe Mbwa Ulaya kuliko kuwa binaadamu Tanzania.
KUTEMBEA NA MABIBI NA MABABU WA KIZUNGU
Vijana wa kiume na wakike wamekuwa wakitembea na watu wenye umri mkubwa kutika nje ya nchi haswa wanaotekea nchi za magharibi kwani wao huhisi ni ufahari kutembea na wazungu,ukipita katika bichi nyingi za nchini Tanzania utajionea haya kwani hata Mzungu asiwe na pesa na umri umeend ila kwa watanzania imekuwa ni fahari kutembea na wazungu.
SABABU YA KUTOKEA HAYO
Ulimbukeni usio na msingi kwani watu huhusi wazungu ni watu ambao wako juu kila kitu wakati si kweli wazungu hao hao ndio ambao baada ya kujisaidi haja kubwa hutumia makaratasi kujisafisha na maji kusafishia choo,Kitu ambacho na sawa na kutembea hali ya kuwa hauko safi.
Kukosa elimu pia huchangia watu kuwapenda wazungu kwa kiwango cha juu na kusahau thamani yao kama watanzania kiasi cha kutamani kuishi huko wanapoishi wazungu kwani hawajui ni mambo mangapi mabaya yalitendwa na wazungu katika zama za ukoloni katika nchi hii ya Tanzania.
ATHARI YA AJALI YA KIFIKRA
Kuzamia kwa vijana wa Tanzania katika nchi kigeni,Watanzania wengi wamekuwa wakitoroka nchini na kuamua kuzamia meli ili kwenda kuishi maisha ya Ulaya kwani wao huhisi huko ndiko maisha yalipo wa hata huko nako kumekuwa na maandamanoa ya mara kwa mara kutokana na hali ngumu ya uchumi kama vile nchini uingereza mwaka juzi kuandamana kama ilivyobainishwa hapa
Kupungua kwa uzalendo nchini,pia hali hii hupelekea vijana kupungua kwa uzalendo na nchi yao kwani siku hujihisi hawapo sehemu stahiki na siku zote hutamani kuondoka nchini na kwenda huko ambako wao huhisi ndio duniani na wala sio hapa Tanzania
HITIMISHO
Tunapaswa kuwa makini na kauli zetu kwani kauli zetu ndio zinajenga kizazi kijacho kihisia na kifikra,Tuwaepushe watotowetu  na JALI YA KIFRA ili kuwafanya kuwa wazalendo pamoja na kuwaambia thamani yao wao wakiwa kama binaadamu katika mahala popote na pia wakiwa kama Watanzania ili kuliinua juu taifa la TANZNIA


Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment